Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, Bw. Masha Mshomba akielezea
malengo ya Mfuko na kazi zake, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tano kwa
madaktari kwenye jengo la LAPF jijini Dar es Salaam Mei 16, 2016. Mafunzo hayo
yanalenga kuwaelimjsha madaktari namna ya kubaini na kushughulikia wahanga wa ajali
na magonjwa yatokanayo na kazi.
NA
K-VIS MEDIA/Khalfan Said
MFUKO
wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwa kushirikiana na Shirika la Kazi Duniani (ILO)
wameanza kutua mafunzo kwa madaktari nchi nzima kuhusu namna ya kubaini na
kushughulikia wahanga wa ajali na magonjwa yanatosababishwa na kazi. Jumla ya
madaktari 380 wa hospitali za rufaa mikoani na wilayani watafaidika na mafunzo
hayo.
Mafunzo
yatatolewa kwa siku tano katika vituo vikubwa vinne ikiwemo Dar es salaam,
Arusha, Mwanza na Mbeya. Wataalamu
kutoka ILO waliobobea katika ajali na magonjwa yanayotokana na kazi Dr. Jacques
Pelletier na Dr. Sylvie Thibaudeau ndio watakaoendesha mafunzo hayo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Bw. Masha Mshomba amesema kwamba mafunzo
haya ni hatua muhimu sana kwa Mfuko kwani Mfuko unaanza rasmi ulipaji wa mafao
tarehe 01 Julai 2016 kwa Wafanyakazi wote watakaopata ajali au magonjwa
kutokana na kazi. Miongoni mwa mafao yataayotolewa ni Huduma ya matibabu, Fidia
kwa ulemavu wa muda, Fidia kwa ulemavu wa kudumu, Ukarabati na ushauri nasaha,
Malipo kwa anayemhudumia mgonjwa, gharama za mazishi endapo mfanyakazi
atafariki na fidia kwa wategemezi endapo mfanyakazi pia atafariki.
Bw.
Masha Mshomba akifafanua dhumuni kubwa la kufanya haya mafunzo alisema, “Kazi
kubwa ya madaktari hawa itakuwa ni kufanya tathimini ya magonjwa yanayotoka na
kazi na kutupa ushauri wa kuendelea na malipo kama wahusika watakuwa wamepata
ajali au kuugua na wakapata ulemavu”
Baadhi ya washiriki wa mafnzo wakifuatilia maelezo ya Mkurugenzi Mkuu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii, SSRA., Bi. Irene Isaka, akitoa hotuba ya ufunguzi
Washiriki
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, Mama Radhmina Mbilinyi
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba
Bi. Isaka na Masha wakiwa kwenye meza kuu wakiandaa hotuba zao
Wataalamu kutoka ILO waliobobea katika ajali na magonjwa yanayotokana na
kazi Dkt. Jacques Pelletier (kulia) na Dkt. Sylvie Thibaudeau wakibadilishana mawazo muda mfupi kabla ya kutoa mada zao
Afisa Mwandamizi wa WCF, Rehema Kabongo, akiwakaribisha washiriki na wageni wengine kwenye mafunzo hayo
Mjumbe wa bodi ya wadhamini ya WCF, Bw. Athuman H. Msengi, akiwasili ukumbini huku akisaidiwa na msaidizi wake.
No comments:
Post a Comment