Tangazo

October 26, 2016

Bayport yajivunia miaka 10 ya kutoa huduma ya mikopo nafuu ya kifedha Tanzania


 Dar es Salaam, 21st  October 2016 –  Taasisi inayoongoza Tanzania kwa kubobea katika kutoa mikopo nafuu, Bayport Financial Services katika kipindi cha miaka 10  iliyopita  imechangia kwa kiwango kikubwa  katika kuboresha maisha ya maelfu ya Watanzania kupitia  utoaji wa mikopo.
 Bayport Tanzania ni miongoni mwa taasisi tanzu kumi za Taasisi ya Bayport Group ambayo hutoa ufumbuzi wa kifedha  kwa watu binafsi walioko katika ajira rasmi au waliojiajiri ndani ya soko linaloibukia. Huduma zinazotolewa na taasisi hiyo  zinaboresha ujumuishwaji kifedha  kwa watu ambao hawana uwezo wa kuzifikia  huduma za kawaida za kibenki  au walio na kiasi kidogo cha fedha katika benki.
Baada ya kuanza shughuli zake  nchini Zambia mwaka 2001, shughuli za Bayport  kwa hivi sasa zinaendeshwa katika nchi saba barani Afrika na  nchi mbili ndani ya Amerika Kusini. Nchi hizo ni Zambia, Uganda, Ghana, Tanzania, Botswana, Afrika Kusini, Msumbiji, Colombia, na Mexico.
 Hivi sasa Bayport  imekuwa ni msingi wa kuaminiwa na mteja ikiwa na  takribani wateja 518,000 ambao  kila mara wamekuwa wakipata  na hata na kufurahia huduma inazozitoa.  
 Kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bayport Tanzania, John Mbaga, Bayport imeshatoa  zaidi ya  shilingi bilioni 48 katika kipindi cha mwaka wa fedha 2015 peke yake. Kwa upande mwingine Bayport inachukuliwa kuwa ni ‘mlipa kodi mkubwa’  nchini Tanzania  ikiwa  imelipa  zaidi ya shilingi bilioni 7 kwa mwaka wa fedha 2014.

“Matamanio yetu ni  kuboresha maisha ya  wateja wetu  na kuwapa fursa  ambazo zitawanufaisha  sio wao peke yao bali pia  watoto wao na kizazi kijacho,” alisema Mbaga  katika mazungumzo yake na wanandishi wa habari hivi karibuni.
Aliongeza, “Tunawasaidia kwa kuangalia unafuu utakaotokana na  mtiririko wa fedha katika kipindi kifupi ambapo matokeo yake  husaidia familia katika kuongeza na kuwa na ustawi wa kifedha  wa kudumu.”
 Bayport Tanzania  ilianzishwa mwaka 2006, na kwa haraka  imekuwa ni  mtoaji wa mikopo kwa wafanyakazi katika sekta za umma na binafsi. Kuwepo kwa ofisi zake 83 za kudumu na matawi 45 ya muda  kumeifanya  kufika kila mkoa kwa Tanzania Bara.
 Kampuni hii ina wafanyakazi wa kudumu 300 na mtandao wa mawakala wa mauzo zaidi ya 1000.
 “Kazi ambazo tumekuwa tunazitoa zimechangia kupunguza ukosefu wa ajira kwa vijana hapa nchini,” anasema Mbaga.
 Kwa mujibu wa utafiti wa Ujumuishaji wa Nguvu Kazi (Integrated Labour Force Survey 2014), kiwango cha ukosefu wa ajira  nchini Tanzania kilikuwa  ni asilimia 13.7.
 Mbali na kutoa mikopo, mambo mengine ambayo Bayport inajishughulisha nayo  ni pamoja na  bidhaa za bima kama vile Sera ya Ulinzi Kielimu ambayo inashughulikia utegemezi wa ada katika elimu kwa muda wa hadi miaka mitatu katika iwapo kwa bahati mbaya mwenye bima  hiyo atafariki. Sera ya Bima ya Maisha ya Bayport inahusisha kulipia salio lililobakia  iwapo wateja watapunguzwa kazi, watakuwa wamepata ulemavu, watafariki au  kupatwa na maradhi kama vile saratani.
 Hivi karibuni Bayport ilizindua  aina ya mikopo kwa ajili ya nyumba ambayo inawawezesha  wateja  kumiliki kiwanja kilichopimwa. Bidhaa hiyo inawezesha Bayport kuifikisha mikopo yake kwa mkopaji kwa  kutumia  kiwanja kilichopimwa kama dhamana.

Akizungumza kuhusu sera ya Bayport kuhusu  kuwajibika kwa huduma za kijamii, Mbaga alisema  kwamba elimu ndio kipaumbele chake. “Kupitia mkakati wa ‘Badilisha Maisha’ tumeshafanya ukarabati wa  madarasa katika shule kadhaa, kutoa msaada wa madawati, kutoa udhamini wa masomo kwa  wanafunzi wa vyuo vikuu pamoja na kutoa msaada wa vitabu. Tangu mwaka 2006, tumetoa misaada ya moja kwa moja kwa wanafunzi 1,500 wa shule za msingi na sekondari.”
 Bayport pia inawasaidia watoto yatima. Mradi wa mfano unajidhihirisha kwa kuisaidia shule ya watoto yatima inayodhaminiwa na Mfuko wa Fursa kwa Wote (EOTF) ambapo Bayport imeboresha  shule hyo ya awali kuwa katika viwango vya kisiasa.
Uwekezaji wa shilingi milioni 200 uliofanywa na Bayport umewezesha kuwepo kwa mazingira rafiki  ukiwepo mwanga wa asili na sehemu asilia za kupitisha hewa kwa ajili ya watoto 40 wanaohudumiwa akatika kituo cha EOTF  na wengine 60  kutoka katika vijiji jirani wakinufaika.
 Akiangazia kuhusu safari ya miaka kumi ya mafanikio katika biashara hapa nchini, Mbaga anasema  kwamba Kampuni hiyo  inajivunia kukua kwake  na kukomaa  ambako imeweza kufikia katika kipindi cha mwongo mmoja uliopita. “Tunasherehekea  fursa hii na  uwezo wa kuleta mabadiliko katika maisha ya wateja wetu, wadau, wafanyakazi na jumuia katika maeneo  tunakoendesha shughuli zetu.”
 Alidokeza kuwa dira ya kimkakati ya taasisi hiyo na utekelezaji wake uliokwishafanyika umejikuta ukipata msaada kutoka kwa wawekezaji, miongoni mwao  ni kampuni ya uwekezaji wa Sweden  ya AB Kinnevik. Julai 2010 kampuni hiyo iliwekeza  dola milioni 40 katika Bayport Group na hivyo kuwa taasisi pekee yenye hisa nyingi ndani ya Bayport.
 Miezi minne baadaye Bayport ilitoa kwa mara ya kwanza katika masoko ya madeni ya mitaji kimataifa  kwa kukusanya jumla ya  dola milioni 100.

“Mwaka 2016 uongozi wa Bayport  uilifikia  dola milioni 250  ikiwa ni uwezo wa salio kubwa  kupatikana kutoka Shirika la Uwekezaji Binafsi Ng’ambo (Overseas Private Investment Corporation-OPIC), ambayo ni  taasisi ya maendeleo ya fedha ya serikali ya Marekani. Mkopo huo wa muda mrefu utasaidia ujumuishwaji wa kifedha  wa taasisi na ajenda yake ya kukua  katika  shughuli zake zote. Kama taasisi tanzu ya Bayport, Bayport Tanzania  inachangia katika historia ya uwekezaji wa taasisi na faida zinazotoka ndani yake.”
 Kwa mujibu wa Mbaga mkakati wa kibiashara wa Bayport upo katika mabadiliko ya bidhaa  na ubunifu wa kiteknolojia  na ‘watu wakiwa ndio nguzo yetu kuu’.
 Ndani ya mkakati huo wa taasisi, Bayport Tanzania mwaka 2015 utambulisho wake ulipata chapa mpya  ikiwa na ujumbe uliojikita kwa watu, na hivyo kuipa taasisi  fursa ya  ya  kujiweka tena yenyewe katika  mtoaji wa ufumbuzi wa kifedha.
“Bidhaa yetu mpya haikuanzishwa katika hali ya upweke. Iliibuka ndani ya falsafa yetu ya kibiashara ambayo inaitwa ‘The Bayport Way”, Mbaga alifafanua  na kuongeza, “Falsafa hiyo  inahusu mambo yote  ya namna tunamchukulia mteja, awe ni mwajiriwa, mteja au mwekezaji, na jinsi ambavyo tunaongeza thamani  katika maisha yao.”
 Kama taasisi Bayport inaamini  kwamba mikopo ni nyenzo yenye nguvu inapotumiwa kistaarabu na katika mazingira yaliyo na ufanisi. “Hakuna kinachotufanya kama pale ambapo tunapowaona wateja wetu  wakiitumia mikopo katika matumizi chanya na kuendesha shughuli za kiuchumi ambazo kimsingi  zinaboresha maisha yao,” Mbaga alisema.
 Ofisa Mtendaji Mkuu huyo aliwashukuru wateja wa Bayport Tanzania, wafadhili, serikali na wadau wengine  kwa kuiunga mkono taasisi hiyo  bila kuchoka  katika kipindi chote cha miaka kumi.
Alisema, “Imekuwa  ni safari ya kuvutia iliyojaa mafanikio. Bila wadau wetu hawa hatungaweza kufikia hatua hiii. Nawahakikishia  kwamba Bayport Tanzania  inaimarika kila mwaka. Wakati tunaelekea katika mwongo mwingine  tumejipanga na tumejikita katika kufanikiwa  hata katika viwango vya hali ya juu vya ufanisi katika kutoa  kutoa bidhaa zisizo na ushindani nchini Tanzania.”

No comments: