Tangazo

October 25, 2016

UN YAADHIMISHA MIAKA 71, YAAHIDI KUWEZESHA VIJANA

WAKATI Umoja wa Mataifa (UN) ukiadhimisha miaka 71 tangu kuanzishwa kwake, imeahidi kuwatumia vijana katika utekelezaji wa malengo yake 17 ya maendeleo.

Mwakilishi Mkazi wa UN nchini, Alvaro Rodriguez amesema ili kufanikisha hilo, UN pamoja na mashirika mengine itatoa mafunzo ya vitendo kwa vijana zaidi ya 50,000 ifikapo mwaka 2017 ambao wataingizwa katika mpango wa utekelezaji wa malengo hayo.

"UN itaendelea kushirikiana na vijana pia itatoa elimu ya vitendo.Hadi sasa vijana zaidi ya elfu kumi wamepewa mafunzo na wanatambua malengo hayo, na kwamba UN na wadau wengine wanatarajia kufundisha vijana zaidi ya 50, 000 ifikapo mwaka 2017, ili ifikapo 2030 vijana wengi wawe wanajua malengo hayo na namna ya kuyatekeleza," amesema.

Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (wa tatu kulia) akiwasili kwenye viwanja vya Karimjee akiwa ameambatana na mwenyeji wake Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Celestine Mushy (kushoto) kwenye sherehe ya kupandisha bendera ya Umoja wa Mataifa katika kuadhimisha miaka 71 ya umoja huo ambapo kila mwaka Oktoba 24 huadhimishwa.(Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog)< /div>

Amesema miongoni mwa mafunzo yatakayotolewa kwa vijana hao ni pamoja na jinsi ya kufanikisha malengo 17 ya maendeleo endelevu ya umoja huo na jinsi ya vijana watakavyoweza kujiajiri.

Aidha, Rodriguez amesema tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana linasababisha umasikini kwa kuwa nguvu kazi hiyo inashindwa kuwajibika katika kuliletea taifa maendeleo.

"Ongezeko la vijana na mahitaji yao ni moja ya changamoto kubwa nchiniTanzania, tunahitaji kuhakikisha kwamba vijana wanawajibika katika kujiendeleza ili kupata maendeleo chanya katika maisha yao, ili kufanikisha hayo vijana wanatakiwa kuwa na ufahamu na taaluma katika kuwezesha mabadiliko ya uchumi nchini Tanzania," alisema Rodriguez na kuongeza: "Vijana wasisahau kuwa wao ni chachu ya amani na maendeleo na UN tutaendelea kushirikiana nao kuhakikisha vijana wanakuwa wadau wa taratibu na kanuni zilizosababisha kuundwa umoja huu, wakijua na kutambua malengo ya dunia," amesema.

Rodriguez amesema UN itaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kuleta maendeleo nchini.
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akitambuliswa kwa Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini Afisa utawala na fedha, Spencer Bokosha (wa pili kulia) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez katika sherehe za maadhimisho ya miaka 71 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa zilizofanyika katika viwanja vya Karimjee jana jijini Dar es Salaam. 

"UN itashirikiana na serikali ya Tanzania kuleta maendeleo ikiwemo kuboresha utoaji wa huduma za kijamii," amesema.

Kwa upande wa mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga amesema serikali inatambua mchango wa umoja huo katika kuleta maendeleo nchini na kwamba itaendelea kushirikiana na umoja huo.

"Serikali ya awamu ya tano tangu kuanza kwake imefanya mambo mengi ili kuleta maendeleo, imedhibiti mianya ya ukwepaji kodi, imefanikiwa kutanua wigo wa ukusanyaji mapato na kuondoa rushwa. Hatuwezi kushinda pekee katika kuleta maendeleo ya wananchi, serikali iko tayari kushirikiana na jumuiya zote duniani," amesema.

Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi nchini (UNHCR), Chansa Kapaya mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Karimjee kwenye sherehe ya kupandisha bendera ya Umoja wa Mataifa katika kuadhimisha miaka 71 ya umoja huo tangu kuanzishwa jana jijini Dar es Salaam.

Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akipokea heshima ya gwaride maalum kwenye sherehe za kupandisha bendera ya Umoja wa Mataifa kuadhimisha miaka 71 ya umoja huo tangu kuanzishwa kwake zilizofanyika katika viwanja vya Karimjee jana jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 71 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake yaliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jana jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akishuhudia kupandishwa kwa bendera ya Umoja wa Mataifa ikiwa ni ishara ya maadhimisho ya miaka 71 ya umoja huo tangu kuanzishwa kwake yaliyofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wakurugenzi wa taasisi mbalimbali, serikali na wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wakitoa heshima kwa wimbo wa Taifa wakati wa kupandishwa kwa bendera ya Umoja wa Mataifa kwenye maadhimisho ya miaka 71 ya umoja huo tangu kuanzishwa yaliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jana jijini Dar es Salaam.

Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akitoa hotuba kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 71 ya Umoja wa Mataifa zilizofanyika katika viwanja vya Karimjee jana jijini Dar es Salaam.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akimpongeza Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga kwa hotuba nzuri.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akitoa salamu za Umoja wa Mataifa kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 71 ya Umoja huo tangu kuanzishwa kwake zilizofanyika katika viwanja vya Karimjee jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya mabalozi mbalimbali waliodhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 71 ya Umoja wa Mataifa wakiwa jukwaa kuu katika viwanja vya Karimjee jana jijini Dar es Salaam.
Meza kuu, kutoka Kulia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni , Katibu Mkuu wa Asasi ya Umoja wa Tanzania (UNA), Reynald Maeda, Brigadia Jenerali (TPDF), Dominic Mrope, Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na Mkuu wa Mabalozi Balozi Prof. Ambrosio Lukoki.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwemo wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa waliohudhuria sherehe za miaka 71 ya Umoja wa Mataifa zinazofanyika Oktoba 24 kila mwaka ambapo jana zilifanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.


Mshehereshaji wa sherehe za maadhimisho ya miaka 71 ya Umoja wa Mataifa, Bertha Makilagi (kushoto) akijadiliana jambo na Nguse Nyerere (kulia) Afisa mwenzake wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika viwanja vya Karimjee jana jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wa shule msingi Uhuru Mchanganyiko wakitoa burudani wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 71 ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika jana katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jitegemee wakitoa buradani katika sherehe za miaka 71 ya Umoja wa Mataifa zilizofanyika jana jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Karimjee.
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga katika picha ya pamoja na waheshimiwa mabalozi na viongozi mbalimbali huku wakiwa na mabango ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) katika sherehe za miaka 71 ya Umoja wa Mataifa zilizofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jana jijini Dar es Salaam.
Jukwaa kuu katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule mbalimbali waliohudhuria maadhimisho ya sherehe za miaka 71 ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jana jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Celestine Mushy (katikati) wakati akijiandaa kuondoka kwenye viwanja vya Karimjee zilipofanyika sherehe za miaka 71 ya Umoja wa Mataifa jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez.
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiagana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez baada ya kumalizika kwa sherehe za kupandisha bendera ya Umoja wa Mataifa ikiwa ni maadhimisho ya miaka 71 ya umoja huo tangu kuanzishwa kwake zilizofanyika katika viwanja vya Karimjee jana jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akiteta jambo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez wakati akijiandaa kuondoka kwenye viwanja vya Karimjee jana jijini Dar es Salaam.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akizungumza jambo na mmoja wa wageni waalikwa kwenye sherehe za kupandisha bendera ya Umoja wa Mataifa ikiwa ni maadhimisho ya miaka 71 ya umoja huo tangu kuanzishwa kwake zilizofanyika katika viwanja vya Karimjee jana jijini Dar es Salaam

No comments: