Tangazo

January 10, 2017

Vijana wajasiriamali watakiwa kutokata tamaa

Jonathan Tarimo (kushoto) kijana mjasiriamali anayejishughulisha na ufugaji  akimwonyesha Afisa Masoko Airtel mkoa wa Arusha, Geoffrey Sayore ndama wa mmoja wa ng’ombe aliyewezeshwa na Airtel kupitia mpango wake wa Airtel FURSA, wakati alipomtembelea ili kujionea maendeleo yake katika Kijiji cha Migungani ‘B’ wilayani Monduli mkoa wa Arusha.

xxxxxxxxxxxxxxxxxx
ARUSHA

 Vijana wanaojishughulisha na ujasiriamali wametakiwa kutokata tamaa na matatizo mbalimbali wanayokumbana nayo wakati wa shughuli zao.

Wito huo umetolewa na mfugaji Jonathan Tarimo, mkazi wa  mkazi wa Migungani kata ya Mto wa Mbu wilaya ya Monduli mkoani Arusha anayejishughulisha na ufugaji

Kijana huyo miezi mitano iliyopita aliwezeshwa kupitia mpango wa Airtel FURSA msimu wa pili kwa kupatiwa ng’ombe wawili, banda la kisasa na mafunzo ya biashara.
  
Akiongea na maofisa wa Airtel waliotembelea katika mradi wake wa ufugaji ili kujionea maendeleo ya biashara yake alisema  kwamba amepata matatizo katika shughuli yake baada ya ng'ombe aliyekuwa anampa maziwa kufa.

“Nawashukuru sana Airtel kwa kunisaidia kufikisha hapa nilipo sasa, maana nlikuwa na ngo’mbe mmoja tu na Airtel kupitia Airtel Fursa kwa kunipatia ngombe wawili ambapo mmoja alizaa na nikawa nauza maziwa kwa wingi lakini baadae alifariki kutokana na ugonjwa. Kwahiyo nikawa nimebakiwa na ng’ombe wawili na ndama. Kwa sasa ndama anaendelea vizuri na huyu ngo’mbe mwingine niliyewezeshwa anamimba. Kwasasa changamoto kubwa ni kutafuta chakula kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa nimekuwa nikienda umbali mrefu ili kupata chakula cha mifugo yangu”.

Alisema, pamoja na adha aliyoipata, aliwaasa vijana wenzangu tusikate tamaa na kuendelea kutafuta fursa mbalimbali zitazoweza kufikisha katika malengo yao hata kama wakipata changamoto mbalimbali

Naye Afisa masoko Airtel mkoa wa Arusha Geoffrey Sayore alisema, Jonathan amekuwa ni mfano mzuri wa kijana aliyewezeshwa na Airtel FURSA na kuweza kupiga hatua kwenye biashara yake pamoja na changamoto mbalimbali zinazomzunguka. 

Aliwataka vijana wanapopata fursa waweze kuzitumia vizuri ili ziwasaidie kuongeza kipato na kutoa ajira kwa jamii inayowazunguka. Lengo letu sisi Airtel ni kuhakikisha vijana wanafaidika na mradi huu wa Airtel Fursa na ndio maaana tunafanya ziara hii kutadhimini mafanikio, changamoto na maeneo ya kuwawezesha zaidi ili kuzifikia ndoto zao na kuwawezesha vijana wengi zaidi.

Airtel FURSA ni mradi wa kijamii kutoka Airtel Tanzania wenye lengo la kuwawezesha vijana wajasiriamali kwa kuwapatia vitendea kazi na elimu ya ujasiriamali ili kuboresha biashara zao.


No comments: