Mmmoja wa Wajasiriamali kushoto
akimuonyesha Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tangaa, Mhandisi Mwanasha Tumbo ambaye
pia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza akiangalia moja kati ya bidhaa
wanazozalisha wakati wa kongamano la wanawake wajasiriamali mkoani Tanga
lililofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga hivi
karibuni.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa
Tanga,Mhandisi Mwanasha Tumbo kushoto aliyevaa hijabu ambaye pia ni Mkuu
wa wilaya ya Muheza akipata maelekezo kutoka kwa mmoja wa wanawake
wajasiriamali wakati alipofungua jukwaa la wanawake mkoani Tanga hivi
karibuni.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa
Tanga,Mhandisi Mwanasha Tumbo ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza
kulia akipata maelekezo kutoka kwa mmoja wa wanawake wajasiriamali
wakati alipofungua jukwaa la wanawake mkoani Tanga hivi
karibuni.
KAIMU Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhandisi
Mwanasha Tumbo ameziagiza wilaya zote za mkoa huu kuunda majukwaa ya
wanawake kwa kipindi cha miezi mitatu ijayo ili yaweze kuwa chachu ya
kuwakomboa kimaendeleo na kiuchumi.
Mhandisi Mwanasha
ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza aliyasema hayo hivi
karibuni wakati akizindua jukwaa la wanawake mkoani Tanga ambalo
litakuwa na malengo makuu ya kuwainua na kuwawezesha wanawake
kiiuchumi lililofanyika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
Alisema uwepo wa majukwaa hayo itasaidia kutoa fursa kwa
wanawake kuweza kushiriki kikamilifu kwenye masuala mbalimbali ikiwemo
kuwepo na majukumu ya kuwawezesha wanawake kuweza kujiinua kiuchumi
kutokana na shughuli wanazozifanya zikiwemo za ujasiriamali.
Aidha pia aliwataka wanawake kuwa mstari wa mbele kuzalisha bidhaa
bora na wenye kiwango cha kimataifa ili waweze kupata nafasi ya
kuziuza ndani na nje ya nchi ili kuwasaidia kuongeza pato lao na Taifa
kwa ujumla.
“Wajasariamali warasimishe biashara zao ili
ziweze kutambulika
kisheria ikiwemo kulipa kodi lakini pia
muachane na suala la
kujiingiza kwenye biashara haramu ambazo
zinaweza kukatisha ndoto zenu “Alisema.
“Kupitia Jukwaa
hili mnaweza mnalitumia kusaidia wanawake kujikwamua kiuchumi na
kuweza kufia sera ya asilimia 50 kwa 50 hivyo ili kufikia huko jukumu
lenu kuonyesha uwezo lakini pia wekezeni kwenye elimu kupitia
mkusanyiko huu “Alisema.
Awali akizungumza Mjasiriamali wa
kampuni ya kutengeneza Fenicha, za majumbani na maofisini mkoani Tanga
Edna Boimanda aliwashauri wanawake kuunganisha nguvu za pamoja ili
kuona namna ya kuanzisha benki ya wanawake kwani hiyo ndio fursa ya
kipekee wanayoweza kujikwamua kiuchumi.
Alisema kupitia
benki hiyo itawawezesha waanawake kujiletea maendeleo kwa kupata
mikopo itakayokuwa chachu ya kufikia malengo yao ya kupata
mafanikio.
Aliwataka kutumia fursa hiyo ya kutengeneza
misingi ya kibiashara
ambayo inaweza kuwasaidia kuondokana na
changamoto ambazo wanakumbana nazo kwenye masuala ya mitaji.
Naye kwa upande wake Mjasiriamali wa Kikundi cha Raha Gani Women
Group Haifa Kijazi aliiomba serikali kuangalia namna ya kuwasaidia
viukundi mbalimbali ili viweze kujikwamua kiuchumi.
“Kwani
ukiangalia leo hii vikundi vingi vimekuwa msaada mkubwa kuwa mkombozi
wa wanawake kwa kuwawezesha kukabiliana na ugumu wa maisha kwa
kuwekeza na kukopa “Alisema.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha
No comments:
Post a Comment