Tangazo

March 16, 2017

Wakulima na wafugaji wa Kata ya Nkiniziwa , Nzega wanufaika na Airtel

Mkuu wa wilaya ya Nzega Godfrey Ngupula (katikati)  akikata utepe kuzindua manara wa mawasiliano wa mwakashahala ulipo kijiji cha Ngukumo kata ya Nkiniziwa Wilayani Nzega ambapo pamoja na mnaro huu Airtel imewasha minara mingine mitatu ya mawasiliano katika kata za Kahamanhalanga , Songambele na Itumba na kuwawezesha wakazi zaidi ya elfu 32 kupata huduma za mawasiliano mkoani Tabora.  wakishuhudia wapili kulia ni  Meneja Mauzo wa Airtel Tabora, Fidelis Lugangila akiwa  pamoja na wajumbe wa serikali ya kijiji cha Ngukumo 

XXXXXXXXXXXXXXX

TABORA

WAKULIMA na wafugaji wa kijiji cha Ngukumo  kata ya Nkiniziwa wilaya ya Nzega mkoani Tabora wameipongeza Airtel kwa kuwezesha upatikanaji wa huduma za mawasiliano ya uhakika na kuwawezesha kuangalia bei za bidhaa na kutafuta masoko kupitia simu zao za mkononi.

Hayo yalisemwa na wakazi wa kijiji cha Ngukumo wakati wa uzinduzi huduma za mawasiliano utakaowawezesha wakazi zaidi ya elfu 32 kutoka katika vijiji 6  kupata huduma za mawasiliano baada ya Airtel kuwasha minara ya mawasiliano  katika maeneo ya Mwakashahalala Kahamanhalanga, Songambele  Itumba mkoani hapo

‘’Tumekuwa tukipata changamoto nyingi sana ikiwemo mawasiiano hafifu ambapo ilibidi kusafiri umbali mrefu kupata huduma za mawasiliano, Tunaishukur kampuni ya Airtel kwa kuona ni vyema kutufikishia huduma za mawasiliano hapa na kutuunganisha na ndugu jamaa  na wafanyabiashara   katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi alisema mkazi wa kata ya Nkiniziwa, John

Akiongea wakati wa uzinduzi, Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Godfrey Ngupula  alitambua na kupongeza juhudi zinazo fanya na Airtel katika kuhakikisha huduma za mawasiliano zinapatikana kwa wote kufatia mchango wake muhimu katika kukuza uchumi wa nchi na kusema ni muhimu kuwa na mawasilino bora kwani kichocheo kikubwa katika kuboresha maisha ya watanzania na kurahisisha shughuli zao za kijamaa na kiuchumi.

“Naamini mawasialiano haya yataweesha biashara katika wilaya hii kukua, na wakulima watanufaika na huduma mbalimbali za simu zitakazowawezesha kutafuta masoko ya bidhaa zao, kuangalia bei ya mazao, lakini pia watatumia huduma ya Airtel Money kwaajili ya kufanya malipo na manunuzi kwa njia ya simu. Nawaasa wakazi wa wilaya ya Nzega kutumia mawasiliano haya vyema na kuboresha maisha yao” aliongeza Ngupula

Kwa upande wake Meneja wa Airtel mkoa wa Tabora, Phidelis Lugangila  alisema “Airtel imejipanga kutoa huduma bora na za uhakika na kuwaomba wakazi wa kijiji cha Ngukumo na vijiji vya jirani kutumia huduma na bidhaa za Airtel kupata kipato  kupitia huduma zetu kama vile Airtel Money kwa kuwa mawakala na kupata kamisheni kila mwezi na vilevile kutengeneza ajira kwa vijana wengi.

Wakazi wa mwashala wanajishughulisha zaidi na kilimo cha mahindi, pamba, Karanga na Mpunga pamoja na ufugaji.

No comments: