IDARA ya Uhamiaji Mkoani Tanga
imewakamata wahamiaji haramu 45 kutoka nchini Ethiopia katika Kijiji cha Horohoro wilayani
Mkinga mkoani Tanga kwa kosa
la kuingia nchini kinyume cha sheria wakiwa shambani kwa wananchi wanakula mahindi kabla
ya kutiwa nguvuni.
Licha ya kukamatwa kwa wahamiaji haramu hao lakini pia idara hiyo inamshikilia raia mmoja kutoka
nchini Kenya ambaye ndio alikuwa
akiwaongoza wahamiaji haramu hapa.
Akizungumza na waandishi wa habari, Afisa Uhamiaji Mkoa wa Tanga, Crispin Ngonyani (Pichani), alisema wahamiaji
haramu hao walikamatwa June 18
mwaka huu katika kijiji hicho baada kupata taarifa kutoka
kwa wasamaria wema wa
eneo hilo.
Alisema wahamiaji haramu hao walikamatwa wakiwa porini katika
jiji hicho wakati wakisafiri
kuelekea nchini Afrika Kusini ambapo
waligunduliwa na wananchi baada ya kufika mashambani mwao
wakawakuta wanakula mahindi
ndio walipotoa taarifa kwa askari wa Polisi wa Horohoro na hivyo wakaenda kuwakamata.
Aliwataja wahamiaji haramu hao kuwa ni Melesa Manesha, Asaf
Erisid,Ashnif Agide,Mulugeta Menano,Demek Sorebeto, Samal
Latbo,Temesgen Tefera,Tememi Juheri,Mubarc Lamago,Temesa
Kibemo,Haftamu Tumiso,Teshum Assfe,Yohanness Ayano na Daniel
Abbate.
Aidha Ofisa Uhamiaji huyo aliwataka wengine walio kamatwa kuwa ni Kibmam Abab,Temesgzeen Ayele,Akilu
Abraham,Pxirose Makore,Munyasha
Lombaso,Berekei Cezenzeni ,Detebo Erikato, Ayele Kebamo,Tamrat
Mamo.
Wengine waliokamatwa kuwa ni Saniel Wolde,Tomiot Deto Gem,Abeje Alemeyo, Ashenaf Waje,Tariko
Dutamo,Birhanu Atso,Tesefaye Dena,Tekel Abush,Tesyfe Landu na Abdi Hassani.
Kwa mujibu wa ofisa uhamiaji huyo aliwataja wengine kuwa ni Daafa Daimo,Getahun Zeleke,Yonas Liliso,
Amanei Ashebo, Xesabo Womago,Isagay
Tikie Mubarik Analo,Begaye Ganorem,Dawit Teso,Teshele
Kemiso,Samweli Hyle na
Tamasgen Sorsa.
Alisema wahamiaji haramu hao wamefikishwa mahakamani jana kujibu tuhuma zinazowakabili akiwemo
msindikizaji Mongela Kidhome ambaye ni Mkenya na mkazi wa mpakani mwa Kenya na Tanzania
Horohoro.
Hata hivyo aliwataka mawakala wa wahamiaji haramu kuacha mara
moja vitendo vya kuwaingiza
nchini kwani watakaobainika watafikishwa kwenye vyombo vya kisheria kujibu tuhuma
zinazowakabili.
Habari kwa hisani ya Blog
ya Kijamii ya Tanga Raha.
No comments:
Post a Comment