Tangazo

July 25, 2017

Benki ya NMB yafungua matawi mapya mikoa mitatu

Mkuu wa Wilaya Itilima –Benson Kilangi (kati kati ) akikata utepe kuzindua rasmi tawi la benki ya NMB Itilima katika Mkoa wa Simiyu. Kutoka kulia ni Kaimu Meneja wa NMB kanda ya Magharibi –Peter Madaha na Mbunge wa Itilima- Njalu Silanga wakishuhudia uzinduzi wa tawi hilo. Tawi hili ni miongoni mwa matawi mengine mawili yaliozinduliwa kwa pamoja katika kanda ya magharibi mwishoni mwa wiki. Mkuu wa Wilaya Igunga –John Mwaipopo (kati kati ) akikata utepe kuzindua rasmi tawi la benki ya NMB Nkinga katika wilaya ya Igunga mkoa wa Tabora wengine pichani ni Meneja wa NMB kanda ya Magharibi Leon Ngowi (wa kwanza kushoto) na Meneja wa NMB tawi la Nkinga Jasmina Tengia (kulia). Tawi hili ni miongoni mwa matawi mengine mawili yaliozinduliwa kwa pamoja katika kanda ya magharibi mwishoni mwa wiki.

  Na Mwandishi Wetu 

  BENKI ya NMB imezidi kung’ara nchini huku ikifanikiwa kutanua mtandao wake kwa kufungua matawi mapya matatu katika mikoa ya Kigoma, Tabora na Simiyu. Uzinduzi wa matawi hayo ulifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo kufunguliwa kwake kutaleta neema kwa wakazi wa maeneo hayo. 

 Mkoani Kigoma benki hiyo ilizindua tawi jipya Wilaya ya Uvinza, Tabora (Igunga) katika mji wa mashuhuri wa Nkinga na Simiyu Wilaya mpya ya Itilima. 

 Awali akizungumza katika uzinduzi wa tawi hilo, Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma, Mwanamvua Mrindoko, aliwataka wananchi wa wilaya hiyo kutumia fursa ya benki hiyo ikiwemo kuhifadhi fedha zao na huduma za kifedha ikiwemo mikopo nafuu inayotolewa na benki hiyo.

 Alisema hatua ya kuzinduliwa kwa tawi hilo la Benki la NMB sasa ni wazi wilaya hiyo itajikwamua kiuchumi ikiwemo wananchi wake kujenga urafiki na benki hiyo kwa kupata huduma bora za kifedha.

 “Kuzinduliwa kwa tawi hili jipya katika Wilaya yetu ya Uvinza sasa ni kielelezo kwamba wananchi wataweza kujikwamua kiuchumi kwa kuwa na urafiki wa karibu na benki ikiwemo kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotolewa,” alisema Mrindoko. 

 Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora, John Mwaipopo, akizinduwa tawi jipya katika mji wa Nkinga alisema ni kielelezo tosha cha wilaya hiyo kupiga hatua kimaendeleo. 

Aidha akifafanua zaidi kwa wananchi waliojitokeza kwenye uzinduzi huo, Mwaipopo alisema hatua hiyo ni ishara nzuri na wananchi wataweza kutumia fursa kidekede zinazotolewa na benki hiyo.

 “Asanteni NMB kwa kufika hapa Nkinga, awali wananchi walikuwa wakitembea umbali mrefu hadi Igunga mjini kutafuta benki lakini sasa huduma za kifedha zitapatikana hapa kupitia benki hii nzuri na bora kutokana na huduma zake,” alisema Mwaipopo. 

 Naye Meneja wa TRA Wilaya ya Nzega, Adolf Mtumbuka, akizungumza katika uzinduzi huo, alisema tawi hilo litasaidia kukusanya mapato ya Serikali ambapo awali wananchi wa Nkinga walilazimika kwenda makao makuu ya wilaya. 

 “Ninapenda sana kuishukuru Benki ya NMB sasa imekuja kufungua milango ya kiuchumi katika eneo hili la Nkinga ambalo lipo Wilaya ya Igunga lakini pia lipo jirani sana na Wilaya ya Nzega. Hivyo kuzinduliwa kwake kutasaidia kukusanya mapato ya Serikali kupitia benki hii ambao pia hukusanya mapato ya Serikali kwa niaba ya TRA,” alisema Mtumbuka. 

 Kutokana na kuimarisha huko kwa mtandao wa benki hiyo Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, Benson Kilangi, alisema kuzinduliwa kwa tawi hilo kutachochea wananchi kuzalisha vizuri na fedha watakazopata watahifadhi benki. 

 “Tunahitaji kuweza ndani ya Wilaya ya Itilima ili wananchi wapate muda wa kutosha katika shughuli za uzalishaji ili kuondokana na umaskini. Hivyo nawaomba wananchi wa Itilima mtumie fursa hii ya Benki ya NMB kwa kisingizio hamna mitaji au hajui mfanyaje.

No comments: