Tangazo

July 27, 2017

TIMU ZA YANGA NA SIMBA U20 ZAJITOLEA KUCHEZA MECHI ZA HISANI KUCHANGIA MFUKO WA UDHAMINI WA UKIMWI

 Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Tume ya Taifa ya kudhibiti UKIMWI Tanzania TACAIDS, Elizabeth Kaganda (katikati) akimkabidhi Jezi Meneja wa Vifaa wa timu ya Yanga, Mohamed Mposo, wakati wa zoezi la kukabidhi vifaa vya michezo kwa ajili ya kushiriki Mechi za Hisani kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI. 

Makabidhiano hayo yamefanyika leo asubuhi ndani ya Ofisi za Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, ambapo mchezo wa kwanza utakuwa ni kati ya Yanga na Mbeya City utakaochezwa leo jioni, na mchezo wa pili utakuwa ni Simba na Tanzania Prisons utakaochezwa kesho na fainali itachezwa siku ya Jumamosi kwa kuzikutanisha timu washindi wa mchezo wa leo na wa kesho. Kushoto ni Mratibu wa Mechini hizo, Emmanuel Petro na Teddy Mapunda (kulia) ni Katibu wa TFF Mkoa wa Mbeya.
  Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Tume ya Taifa ya kudhibiti UKIMWI Tanzania TACAIDS, Elizabeth Kaganda (katikati) akimkabidhi Jezi Meneja wa timu ya Mbeya City, Geofrey Katepa, wakati wa zaoezi la kukabidhi vifaa vya michezo kwa ajili ya kushiriki Mechi za Hisani kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI. Kushoto ni Mratibu wa Mechini hizo, Emmanuel Petro na Teddy Mapunda (kulia) ni Katibu wa TFF Mkoa wa Mbeya.
 Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Tume ya Taifa ya kudhibiti UKIMWI Tanzania TACAIDS, Elizabeth Kaganda (katikati) akimkabidhi Jezi Meneja timu ya Tanzania Prisons, Havinitishi Abdallah (wa pili kulia) wakati wa zaoezi la kukabidhi vifaa vya michezo kwa ajili ya kushiriki Mechi za Hisani kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI.. Kushoto ni Mratibu wa Mechini hizo, Emmanuel Petro na Teddy Mapunda (kulia) ni Katibu wa TFF Mkoa wa Mbeya.
 Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Tume ya Taifa ya kudhibiti UKIMWI Tanzania TACAIDS, Elizabeth Kaganda (wa pili kushoto) akimkabidhi Jezi Meneja timu ya Simba SC, Nico Nyagawa (wa pili kulia) wakati wa zaoezi la kukabidhi vifaa vya michezo kwa ajili ya kushiriki Mechi za Hisani kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI.Kushoto ni Mratibu wa Mechini hizo, Teddy Mapunda (kulia) ni Katibu wa TFF Mkoa wa Mbeya.
Na Ripota wa Mafoto Blog, Mbeya

TIMU za Yanga na Simba, U20 zimewasili jijini Mbeya kwa ajili ya kushiriki mechi za Hisani maalumu kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, zinazoanza kutimua vumbi jioni ya leo kwenye Uwanja wa Sokoine jijini hapa. 
Akizungumzia maandalizi ya mechi hizo Msemaji wa TACAIDS na Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Tume ya Taifa ya kudhibiti UKIMWI Tanzania TACAIDS, Elizabeth Kaganda, alimesema kuwa timu za Yanga na Simba kutoka jijini Dar es Salaam, tayari zimewasili jijini hapa, na zipo katika hali nzuri kwa mechi hizo.

''Tunashukuru mungu timu zote zimefika salama kwa ajili ya kushiriki mechi hizo za Hisani kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, na tunatarajia kupata burudani safi ya soka kutoka kwa timu zote kutokana na maandalizi waliyofanya, ambapo mshindi atakabidhiwa kikombe, ambapo timu zote zimejitolea kushiriki bila malipo''. amesema Kaganda 

Aidha alisema mchezo wa kwanza utaanza leo kwa kuzikutanisha timu za Yanga na Mbeya City, na kesho itakuwa ni Simba na Tanzania Prisons, fainali itachezwa siku ya Jumamosi ambapo mshindi wa mchezo wa leo atacheza na mshindi wa mchezo wa kesho, na mechi zote zikipigwa katika Uwanja wa Sokoine majira ya saa tisa na nusu.

No comments: