Meneja Mauzo Airtel Tanzania kanda ya Rukwa Hudson Kamenya
(katikati) na Mbunge wa Jimbo la Kalambo mkoani Sumbawanga wakimkabidhi Mwalimu
wa somo la Kemia kwenye shule ya sekondari ya Mwazye Aidin Mwaibabu baadhi ya
vitabu vilivyotolewa na kampuni ya Airtel Tanzania kwa shule za sekondari zenye
uhaba wa vitabu vya sayansi kwenye Jimbo la Kalambo.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
SUMBAWANGA
Ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali ya
awamu ya tano ya kuhakikisha kila mtoto kuanzia chekechekea mpaka kidato cha
nne wanapata elimu bure, kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania leo imetoa
vitabu vya sayansi kwa shule za mkoa wa Sumbawanga vyenye thamani ya shilingi
milioni kumi TZS 10,000,000.
Vitabu hivyo vimepokelewa na Mbunge wa Jimbo la
kalambo Mh, Josephat Kandege na kugaiwa kwa shule zenye uhabu wa vitabu jimboni
humo.
Akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi
vitabu, Mbunge wa Jimbo la kalambo Mh, Josephat Kandege alisema “ muhimu
kutambua mchango wa makampuni binafsi kama Airtel Tanzania kwa juhudi za dhati
za kuunga mkononi serikali yetu katika kuninua sekta ya elimu hapa nchini. sote
tunajua ya kwamba serikali yetu inaongozwa na sera ya serikali ya viwanda. Kwa
maana hiyo hatuwezi kuwa na viwanda bila ya kuwa na wanasayansi, hiyo basi
vitabu hivi vitaongeza chachu kwa wanafunzi wetu wa kuendelea kufanya vizuri
katika masomo ya sayansi na hatimaye kufanikisha ndoto zao pamoja na serikali”.
Mh Kandege aliendelea kusema kwamba “nawaomba
Airtel na wadau wengine waendelee kutusaidia kwenye nyaja zingine mbali mbali
ili kuendelea kutengeneza mazingira bora kwa wanafunzi kujifunza na hivyo
kuongeza uelewa na kuwa na taifa lenye ueledi”.
Kwa upande wake Meneja Mauzo wa Airtel Rukwa na
Katavi Bw, Hapson Kamanya alisema “Airtel tunaamini jamii iliyoelimika
inajengwa kutoka katika shule zenye vifaa vya kufundishia vya kutosha hususani
vitabu, ili kuwa na maendeleo endelevu ni muhimu kuwekeza kwenye elimu na
leo tunathibitisha dhamira yetu kwa kutoa msaada wa vitabu katika shule hizi”.
Tunaamini ya kwamba msaada wa vitabu utachochea
ufaulu mzuri katika masomo ya sayansi katika mkoa na pia utaongeza idadi
ya wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi” Aliongeza Kamenya.
Kwa upande Mkuu wa shule ya Mwazye Bw, Haron
Mwaibabu akiongea kwa niaba ya shule zilizofaidika na msaada wa vitabu hivyo
alisema “Msaada huu umekuja wakati muafaka wakati shule zetu zimekuwa na
upungufu wa vitabu na tunaahidi kuvitunza na kuvitumia ipasavyo".
Aliongeza, ni ukweli kuwa shule zetu zina uhaba
wa vitabu vya sayansi kitu ambacho kilikuwa kinatupa ugumu kwenye kufundisha na
hata kupelekea baadhi ya wanafunzi wetu kutotamani kuchukua masomo ya sayansi.
Tunashukuru sana Airtel kwa kuwa mkombozi kwenye hili’.
|
No comments:
Post a Comment