Tangazo

August 9, 2017

Dk. Kigwangalla aagiza TAKUKURU kuwahoji waliokuwa viongozi wa TASO Kanda ya Mashariki

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama mkoa wa Morogoro kuwakamata mara moja waliokuwa viongozi wa chama cha wakulima Tanzania TASO kanda ya mashariki kutokana na ubadhirifu wa fedha walioufanya kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita. 

Dk Kingwangala alitoa agizo hili mara baada ya kupokea taarifa za kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Mh. Dk. Steven Kebwe juu ya walioukuwa viongozi wa Taso kanda ya Mashariki kushirikiana kuuza baada ya maeneo kwa wananchi ndani ya uwanja wa maonyesho ya mwalimu Juliaus Nyerere nanenane ulipo mkoani Morogoro. 

Dk. Kigwangalla ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kilele hicho cha Nane nane akimwakilisha Makamu wa Rais Mama Samia Salum, ameagiza kuchukuliwa hatua za haraka viongozi hao huku akieleza kuwa kutokana na usajili wamashirika yasiyokuwa ya kiserikali kuwa ndani ya wizara yake ni, vyema viongozi hao wakatafutwa na kukamatwa ili waweze kujibu tuhuma zinazowakabili.

“Kwa mamlaka, tunawaagiza Mkuu wa TAKUKURU kuhakikisha wanawakamata viongozi wa TASO haraka ilikuweza kurudisha mali zote ikiwemo walizowauzia wananchi viwanja ndani ya maeneo haya. Taasisi ama NGO’s zikifilisiwa mali zote ni za Serikali na zinakuwa chini ya uangalizi wa Serikali hivyo hatua kali zitachukuliwa kwa wale waote waliohusika” alieleza Dk. Kigwangalla katika tukio hilo la kufunga kilele cha maadhimisho ya Nane nane, Kanda ya Mashariki inayohusisha mikoa ya Morogoro, Tanga, Pwani na Dar e s Salaam, katika Banda la Mwalimu Julius Nyerere. 

Dk. Kigwangalla apia ameweza kutoa zawadi mbalimbali kwa washindi ikiwemo Vyeti, hundi za fedha pamoja na vikombe vya ushindi kwa taasisi na mashirika na wadau walioshiriki maonyesho hayo. Hata hivyo Dk. Kigwangalla ameongeza siku mbili zaidi kuendelea kwa maonyesho hayo ambayo yaendelea leo na kesho Alhamisi Agosti 10,2017. 

Awali amepata Dk. Kigwangalla aliweza kutembelea mabanda mbalimbali ndani ya viwanja hivyo huku akijionea mazao ya kilimo na ufugaji wa kila aina pamoja na bidhaa zitokanazo na kilimo za wadau wa ndani.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akipokelewa wakati akiwasili viwanja vya maonyesho ya Nane nane Kanda ya Mashariki inayohusisha mikoa ya Morogoro, Tanga, Pwani na Dar es Salaam wakati alipokuwa mgeni rasmi kilele cha Nane nane, 8 Agosti 2017
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia namna mashine ya kukoboa mahindi ya kisasa inavyofanya kazi ambayo itakuwa msaada kwa wakulima hapa nchini kwenye viwanja vya maonyesho ya Nane nane Kanda ya Mashariki inayohusisha mikoa ya Morogoro, Tanga, Pwani na Dar es Salaam wakati alipokuwa mgeni rasmi kilele cha Nane nane, 8 Agosti 2017
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia bidhaa za usindikaji kutoka kwa wakulima wa ndani hapa nchini kwenye viwanja vya maonyesho ya Nane nane Kanda ya Mashariki inayohusisha mikoa ya Morogoro, Tanga, Pwani na Dar es Salaam wakati alipokuwa mgeni rasmi kilele cha Nane nane, 8 Agosti 2017
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiwasabahi baadhi ya watoto waliofika kwenye kwenye viwanja vya maonyesho ya Nane nane Kanda ya Mashariki inayohusisha mikoa ya Morogoro, Tanga, Pwani na Dar es Salaam wakati alipokuwa mgeni rasmi kilele cha Nane nane, 8 Agosti 2017
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia bidhaa za usindikaji kutoka kwa wakulima wa ndani hapa nchini kwenye viwanja vya maonyesho ya Nane nane Kanda ya Mashariki inayohusisha mikoa ya Morogoro, Tanga, Pwani na Dar es Salaam wakati alipokuwa mgeni rasmi kilele cha Nane nane, 8 Agosti 2017
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mh. Ally Hapi kwenye viwanja vya maonyesho ya Nane nane Kanda ya Mashariki inayohusisha mikoa ya Morogoro, Tanga, Pwani na Dar es Salaam wakati alipokuwa mgeni rasmi kilele cha Nane nane, 8 Agosti 2017
Baadhi ya viongozi wakiangalia bidhaa za ngozi kutoka kwa Mjasiriiamali kutoka Tanga kwenye maonyesho hayo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia mazao ya shambani kutoka kwa wakulima wa ndani hapa nchini kwenye viwanja vya maonyesho ya Nane nane Kanda ya Mashariki inayohusisha mikoa ya Morogoro, Tanga, Pwani na Dar es Salaam wakati alipokuwa mgeni rasmi kilele cha Nane nane, 8 Agosti 2017
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia mazao ya shambani kutoka kwa wakulima wa ndani hapa nchini kwenye viwanja vya maonyesho ya Nane nane Kanda ya Mashariki inayohusisha mikoa ya Morogoro, Tanga, Pwani na Dar es Salaam wakati alipokuwa mgeni rasmi kilele cha Nane nane, 8 Agosti 2017
Moja ya bwawa la Samaki la kisasa
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia moja ya mabwawa ya samaki ya kisasa kutoka kwa wakulima wa ndani hapa nchini kwenye viwanja vya maonyesho ya Nane nane Kanda ya Mashariki inayohusisha mikoa ya Morogoro, Tanga, Pwani na Dar es Salaam wakati alipokuwa mgeni rasmi kilele cha Nane nane, 8 Agosti 2017
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo namna ya upandaji wa mazaoo ya miwa maalum kwa sukari kutoka kwa wakulima wa ndani hapa nchini kwenye viwanja vya maonyesho ya Nane nane Kanda ya Mashariki inayohusisha mikoa ya Morogoro, Tanga, Pwani na Dar es Salaam wakati alipokuwa mgeni rasmi kilele cha Nane nane, 8 Agosti 2017
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akihutubia katika tukio hilo kwenye viwanja vya maonyesho ya Nane nane Kanda ya Mashariki inayohusisha mikoa ya Morogoro, Tanga, Pwani na Dar es Salaam wakati alipokuwa mgeni rasmi kilele cha Nane nane, 8 Agosti 2017
Baadhi tya viongozi mbalimbali pamoja na wadau wa kilimo wakifuatilia tukio hilo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikabidhi vyeti kwa washiriki kwenye viwanja vya maonyesho ya Nane nane Kanda ya Mashariki inayohusisha mikoa ya Morogoro, Tanga, Pwani na Dar es Salaam wakati alipokuwa mgeni rasmi kilele cha Nane nane, 8 Agosti 2017
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikabidhi kombe la ushindi kwa washiriki kwenye viwanja vya maonyesho ya Nane nane Kanda ya Mashariki inayohusisha mikoa ya Morogoro, Tanga, Pwani na Dar es Salaam wakati alipokuwa mgeni rasmi kilele cha Nane nane, 8 Agosti 2017
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akijadiliana na wadau wa Kilimo hapa nchini kwenye viwanja vya maonyesho ya Nane nane Kanda ya Mashariki inayohusisha mikoa ya Morogoro, Tanga, Pwani na Dar es Salaam wakati alipokuwa mgeni rasmi kilele cha Nane nane, 8 Agosti 2017

No comments: