Na Binagi Media Group
Kampuni ya
Bima ya BUMACO imeilipa kampuni ya mabasi ya BATCO inayofanya safari zake katika
ya mikoa ya Mara na Mwanza, kiasi cha shilingi Milioni 140 ikiwa ni malipo ya
bima baada ya basi la kampuni hiyo kupata ajali ya moto.
Halfa ya
kukabidhi hundi ya fedha hizo imefanyika leo kwenye ofisi za kampuni ya Bumaco
zilizopo Jijini Mwanza, na kushuhudiwa na wageni mbalimbali akiwemo Meneja wa
Mamlaka ya Bima Kanda ya Ziwa ambaye alikuwa mgeni rasmi.
Meneja wa
kampuni ya Bumaco Kanda ya Ziwa, Godlisten Muro amesema kampuni hiyo imekuwa
ikilipa madai ya bima kwa wakati, lengo ikiwa ni kuwanusuru wateja wake na
majanga mbalimbali yanayowakabiri na hivyo kuwataka wananchi kuondoa dhana
kwamba bima hazilipi.
Meneja wa
Mamlaka ya Bima Kanda ya Ziwa, Sharif Ali Hamad ameipongeza kampuni ya bima
Bumaco kwa namna inavyolipa kwa wakati fidia za wateja wake na hivyo kuwasihi
wananchi wakiwemo wafanyabiashara kujiunga na mfumo wa bima ili kunufaika na
fidia pindi wapatapo majanga.
“Basi la
Batco lilipata ajali tarehe 10.06.2017 na leo tarehe 08.09.2017 wanalipwa fidia
ya shilingi Milioni 140, ukiangalia tangu kupata ajali hadi kulipwa fidia ni kipindi
cha miezi mitatu”. Amesema Hamad na kuongeza kwamba hatua hiyo inaonesha ni
jinsi gani kampuni ya Bumaco inavyoshughulikia kwa haraka madai ya wateja wake.
Mkurugenzi wa kampuni ya mabasi ya Batco, Baya
Kusanja Maragi amewasihi wafanyabiashara wenzake kujiunga na kampuni ya bima ya
Bumaco kwani imekuwa ikimlipa kwa wakati madai yake ya bima, ambapo pia tarehe
14.02.2015 basi lake lilipata ajali na akalipwa madai yake ndani ya kipindi cha
miezi mitatu.
Meneja wa Mamlaka ya Bima Kanda ya Ziwa, Sharif Ali Hamad, akionyesha hundi halisi ya malipo kutoka kamouni ya bima ya Bumaco kwa ajili ya kampuni ya mabasi ya Batco ambayo basi lake liliungua moto mwezi wa sita mwaka huu.
No comments:
Post a Comment