NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
SHIRIKA
la Umeme Tanzania, (TANESCO), limekabidhi majengo mawili ya nyumba za walimu,
shule ya sekondari Mtera DAM, iliyoko jirani na Bwawa la kufua umeme wa maji
Mtera, (Mtera Hydro Power Plant), lililoko katikati ya mikoa ya Dodoma na
Iringa.
Nyumba
hizo zilizogharimu shilingi milioni 35, moja ikiwa mpya na nyingine
imekarabatiwa, zimekabidhiwa kwa uongozi wa Wilaya ya Mpwapwa Septemba 6, 2017
na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO anayeshughulikia usambazaji umeme na
huduma kwa wateja, Bi. Joyce Ngahyoma, ambaye alimwakilisha Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi, Dkt. Tito Mwinuka.
Akizungumza
kabla ya kukabidhi nyumba hizo, Bi. Joyce Ngahyoma alisema, wakazi wa kata ya
Mtera ni wadau na washirika wakubwa wa TANESCO katika kulinda miundombinu ya
umeme ya kituo cha kufua umeme cha Mtera ambayo ina gharama kubwa kwa hivyo
walipowasilisha maombi ya kujengewa nyumba ya mwalimu Mkuu, TANESCO ilikubali
ombo hilo bila kusita.
Alisema,
uongozi wa TANESCO baada ya kupokea maombi hayo ulifanya tathmini na kutoa
kiasi cha fedha shilingi Milioni 35 ambazo zilitumika kujenga nyumba jipya na
kukarabati nyumba nyingine.
Nyumba
mpya iliyojengwa na TANESCO kwa ajili ya makazi ya Mwalimu Mkuu, ina vyumba
vinne, choo, bafu na jiko, alisema.
“Napenda
nichukue fursa hii kuwashukuru wananchi kwa ushirikiano mkubwa mnaotupatia na
niwaahidi tu kwamba Shirika litaendelea kushirikiana na serikali na jamii kwa
ujumla katika kuhakikisha sekta ya elimu, afya na huduma nyingine zinaimarika
kwa kutoa michango ya hali na mali.”
Alisema Bi. Ngahyoma.
Alisema,
sambamba na msada huo, TANESCO imekuwa ikisaidia jamii ya wana Mtera, katika
kuwapatia huduma ya afya kwenye zahanati ya wafanyakazi, huduma ya elimu ya
awali(chekechea), kwenye shule ya chekechea iliyojengwa kuhudumia watotot wa
wafanyakazi, na pia usafiri, ambapo mabasi yanayochukua wafanyakazi kwenda na
kutoka kazini, huwasaidia pia wananchi.
Aidha
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia ufuaji umeme, Mhandisi
Abdallah Ikwasa, alisema, Kituo cha kufua umeme wa maji Mtera, kilijengwa
kuanzia mwaka 1984 na kukamilika mwaka 1988 na kuwa na uwezo wa kufua umeme
Megawati 80 na tangu kipindi hicho hadi hivi sasa, TANESCO imekuwa
ikishirikiana na wananchi katika kulinda miundombinu ya kituo hicho.
Mnamo
mwaka 2005 na 2006, Shirika lilichangia kiasi cha shilingi milioni 34 kujenga
madarasa mawili mapya na ujenzi wa ofisi ya walimu, alisema Mhandisi Ikwasa.
Akizungumza
katika hafla hiyo kabla ya kupokea majengo hayo, Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa,
Mhe. Jabir Shekimweri, amewataka wananchi wa Kata ya Mtera, kuendelea kushirikiana na TANESCO, katika
kulinda miundombinu ya Shirika hilo kwenye bwawa la kufua umeme wa maji la
Mtera, (Mtera Hydro Power Plant).
“Ndugu
zangu msada huu umekuja kutokana na faida inayopatikana kutokana na miundombinu
hiyo, kwa hivyo niwaombe muendelee kushirikiana na TANESCO na viongozi wa
serikali ya kijiji katika kuhakikisha usalama wa miundombinu hiyo unaendelea
kuwepo kwani wafanyakazi wa TANESCO pekee hawawezi kulinda miungdominu hiyo peke
yao kwa sababu eneo ni pana sana.” Alifafanua.
Mhe.
Shekimweri alisema, msada wa majengo hayo, utasaidia kutatua changamoto ya
nyumba kwa walimu ambao kutokana na uhaba mkubwa wa nyumba walimu wanaishi
maeneo ya mbali na shule na hivyo inapelekea utendaji kazi wao kuwa wa chini.
“Nimeambiwa
kuwa ufaulu kwenye shule hii ni mzuri na walimu wakiishi maeneo ya karibu na
shule, basi ufaulu huo bila shaka utaongezeka sana.” Alisema.
Lakini
pia niwaombe wananchi, umeme unaopatikana hapa unategemea sana uwepo wa maji,
kwa hivyo nitoe rai, ni lazima tutumie maji haya kwa busara kubwa naelewa zipo
shughuli za uvuvi lakini uvuvi mwingine ni ule haramu wa uharibifu, niwajulishe
tu hivi karibuni tutakaa kikao ili kuweka matumizi bora ya maji haya ili kuzuia
athari zinazoweza kupelekea uharibifu wa vyanzo vya maji yanayoletwa kwenye
bwawa hili, alisisitiza.
Mkuu
huyo wa wilaya aliishukuru TANESCO kwa kuisaidia serikali katika kukabiliana na
changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii kwenye eneo hilo na .
“
Nimeambiwa kuwa sio tu mmesaidia ujenzi wa nyumba moja mpya na kukarabati
nyingine lakini pia mmekuwa mkisaidia wananchi katika kuwapatia huduma za afya
kwenye zahanati ya wafanyakazi, hali kadhalika mmekuwa mkiwasaidia wananchi
katika usafiri ambapo wamekuwa wakitumia usafiri wa wafanyakazi wenu, hili ni
jambo jema katika kujenga mahusiano mema baina yenu na wananchi.” Aliongeza Bw.
Shekimweri.
|
No comments:
Post a Comment