Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) Dkt. Stephen Nindi akielezea kwa ufupi malengo ya warsha kwa ajili ya kurejea mwongozo wa upangaji,utekelezaji na usimamizi wa mipango ya matumizi ya ardhi ya Wilaya, Mjini Morogoro
Kaimu Mkurugenzi wa Uratibu,Sera na Mawasiliano wa Tume Bi. Albina Burra akitoa maelezo mafupi kwa Mkurugenzi wa NLUPC Dkt. Stephen Nindi kuhusiana na kazi ya kurejea mwongozo wa upangaji,utekelezaji na usimamizi wa mipango ya matumizi ya ardhi ya Wilaya.
Makundi mbalimbali ya wana kikao kazi wakiwa wana rejea mwongozo wa upangaji,utekelezaji na usimamizi wa mipango ya matumizi ya ardhi ya Wilaya kabla ya kutoa mrejesho
Bw. Eugine Cylio Mtaalam kutoka NLUPC akitoa mawasilisho kwa niaba kundi lake.
Bw. Paulo Tarimo kutoka Wizara ya Kilimo akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa kusikiliza mrejesho wa majadiliano yaliyokuwa yanaendelea kutoka katika makundi mbalimbali.
Afisa Programu kutoka Haki Ardhi Bw. Joseph Chiombola akitoa mawasilisho kwa niaba kundi lake.
Bw. Angolile Rayson kutoka PELUM Tanzania akitoa mawasilisho kwa niaba kundi lake.
Afisa Miradi kutoka TNRF Bw. Daniel Ouma akichangia jambo kuhusu matumizi ya Ardhi na maendeleo endelevu.
Afisa Sheria wa NLUPC Bi. Devotha Selukele akichangia jambo juu ya 'Participatory Land use Management' (PLUM)
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Ufugaji Tanzania Bw. Joshua Lugaso (wa pilikulia) akichangia jambo kuhusu wafugaji wakati wa kikao kazi.
Afisa Takwimu kutoka NLUPC Bi. Blandina Mahudi akichangia jambo kuhusiana na maswala ya Takwimu.
Baadhi ya watumishi kutoka NLUPC, kuanzia kushoto ni Afisa Mipango Bw. Gerald Mwakipesile, Afisa Sheria Bi. Devotha Selukele, Afisa Tawala Bi. Nakivona Rajabu na Afisa Habari Bw. Geofrey Sima wakati wa Kikao kazi
Tume
na wadau mbalimbali kutoka Serikalini,Asasi za kiraia wamekutana Morogoro
kwa ajili ya kutengeneza urejewa mwongozo wa upangaji,utekelezaji na usimamizi
wa mipango ya matumizi ya Ardhi ya Wilaya.
Akizungumza
wakati wa mchakato huo Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya mipango na Matumizi
ya Ardhi(NLUPC) Dkt. Stephen Nindi alisema kuwa NLUPC ikishirikiana na
Haki Ardhi pamoja na wadau mbalimbali wanaojihusisha na upangaji,
utekelezaji wa usimamizi wa mipango ya ardhi wamekutana kwa ajili ya
kuanza kupitia namna ya upangaji wa matumizi ya Ardhi ya Wilaya ambapo mwongozo
huo uliandaliwa tangu mwaka 2006.
“Kutokana
na mambo mengi kutokea kwa muda wa miaka kumi na moja (11), ambayo
tungependa yawepo katika muongozo huu wa namna ya kuandaa mipango ya
matumizi ya ardhi ya Wilaya, mambo hayo yaliyojitokeza ni kama mabadiliko ya
tabianchi na athari zake kuwa kubwa inayopelekea mabadiliko ya hali ya
kimazingira, ushirikishwaji wa jinsia pamoja na makundi mengine madogo madogo
mfano watu wanaotegemea mizizi na wanaohama hama toka sehemu moja kwenda sehemu
nyengine” Alisema Dkt. Nindi.
Aliongeza
kuwa Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mh. Dkt John Pombe Magufuli anayesisitiza kuwa Nchi iwe ya
viwanda na uchumi wa kati, na katika muongozo wa kuandaa mpango wa
matumizi ya ardhi ya Wilaya haukuupa msukumo wa viwanda. Mwongozo huu
utaangalia utaratibu wa namna gani viwanda vitaendelea katika ardhi
ya Wilaya na vijiji.
Kutokana
na mabadiliko mbalimbali yaliyotokea nchini yakiwomo ya
kiuchumi,kisiasa,kijamii,na ndani ya miaka hii kumi na moja kumekuwa na ukuaji
wa mashamba ya saizi ya kati ekali 100 hadi 150 umeongezeka ambapo unahitaji
muongozo mpya na namna ya kusimamia katika ngazi ya Wilaya,Miji mingi
watu wamezidi kuongezeka ambapo ukuaji huo unaonekana haukutiliwa mkazo wakati
wa mwongozo wa awali ulio andaliwa miaka 11 iliyopita,ambapo sasa kuna kasi ya ongezeko ya ukuaji wa miji na vijiji, mwongozo huu utaangalia namna gani mambo haya
yote yataendelezwa vizuri.
Kwa
upande wake Afisa Programu kutoka Haki Ardhi Bw. Joseph Chiombola ambao
wanajihusisha na utafiti pamoja na utetezi wa maswala ya ardhi alisema kuwa
Haki Ardhi ni jukwaa ambalo limekuwa likiendesha mijadala mbalimbali
inayohusiana na maswala ya ardhi nchini Tanzania, na kwamba maswala ya matumizi
ya ardhi yanahitaji mjadala mpana unaotakiwa kuwahusisha wananchi kwa ujumla.
“Moja
ya malengo yetu ni pamoja na kuhakikisha kwamba kunafanyika mabadiliko ya
Sera,Sheria,kanuni na miongozo mbalimbali, na hili swala la mipango na matumizi
ya ardhi ni sehemu moja tunayo iangalia kwa sababu kama ikiendelezwa ipasavyo
itasaidia kuweka ulinzi wa ardhi na wazalishaji wadogo ambayo ndio jukwaa
tulilokuwa tukizungumzia sana kwa ajili ya haki zao kwa kipindi chote cha uwepo
wetu” alisema Chiombola.
Aliongeza
kuwa mipango hii ni muhimu kwa sababu inawagusa wazalishaji wa kila siku
wakiwemo wakulima,wafugaji, waokota matunda,warina asali na wavuvi kwa kuwa wamekuwa
wanahusika na ardhi kwa namna moja au nyengine. Hivyo mipango itakayokuwa kwa
manufaa ya jamii hizo itakuwa na manufaa makubwa katika kuongeza kipato chao na
kubadilisha hali ya maisha yao.
Nae
Naibu Katibu Mkuu wa wa Chama cha Wafugaji Tanzania Bw. Joshua Lugaso alisema
kuwa kutengeneza urejewa mwongozo wa upangaji,utekelezaji na usimamizi wa
mipango ya matumizi ya Ardhi ya Wilaya utakuwa ni mkombozi kwa mfugaji
kutambulika katika maswala ya ardhi Tanzania jambo ambalo halijawahi kutokea
kwa miaka mingi.
“Katika
mwongozo huu mfugaji ameonekana sana na kuondoa dhana ya kila wakati wakulima
kuonekana, tunaamini kwamba ni mpango unaoenda kufanya kazi kwenye Wilaya
tunaamini kwamba ikisimamiwa vizuri, migogoro ya wafugaji na wakulima
itakwisha” alisema Lugaso.
Katika
mwongozo uliopita kulikuwa na mapungufu ambayo ni pamoja na mkazo wa
namna ya jamii zinavyokabiliana na mabadiliko ya Tabianchi haukuwa na
mkazo mkubwa,hakukuwa na mkazo wa namna ya ardhi za Wilaya zinavyopangwa ili
kuhakikisha kwamba kunakuwa kuna ukuwaji wa viwanda katika ardhi ya wilaya au
ya vijiji, pia swala la ushirikishwaji katika upande wa jinsia na makundi
madogo madogo wanaotumia ardhi ambao katika jamii hawana nguvu ya
kisiasa,kiuchumi kwa kuwa na wao wanatakiwa watambuliwe.
No comments:
Post a Comment