Tangazo

October 28, 2011

MFUKO WA BIMA YA AFYA WAFANYA KONGAMANO LA WANAHABARI -MOROGORO

Wachora vibonzo Nathan Mpangala (kulia) na King Kinya wakisikiliza kwa makini wakati wa kongamano likiendelea.

Baadhi ya wahariri wa habari na waandishi waandamizi  wakiwa katika kongamano la saba la mwaka la kujadili taarifa za utafiti wa huduma za NHIF nchini, lililoanza jana mjini Morogoro.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (kulia), akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari,baada ya kufungua kongamano la saba la mwaka la wahariri wa habari na waandishi waandamizi la kujadili taarifa za utafiti wa huduma za NHIF nchini. Kongamano hilo la siku mbili lilianza jana mjini
Morogoro.

Beda Msimbe wa magazeti ya Serikali ya Daily News na Habari Leo, akitoa taarifa ya utafiti wa huduma zitolewazo na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), katika Mkoa wa Ruvuma.


Mwandishi wa Habari, Joshua Joel akifafanua jambo alipokuwa akitoa katika kongamano hilo taarifa ya utafiti wa upatikanaji wa huduma za afya zitolewazo na NHIF, katika mikoa ya Rukwa na Katavi.

Mwandishi wa habari mwandamizi wa gazeti la Jambo akitoa taarifa ya utafiti wa Leo, Grace Michael huduma za afya zilitolewazo na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), katika Mkoa wa Kigoma.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (kulia)  akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Emmanuel Humba (kushoto) na  Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya mfuko huo, Ally Kiwenge (wa pili kushoto) baada ya kufungua  kongamano la saba la mwaka la wahariri wa habari na waandishi waandamizi la kujadili taarifa za  utafiti wa huduma za NHIF nchini. Kongamano hilo  la siku mbili lilianza jana mjini Morogoro.

No comments: