Tangazo

April 25, 2018

KUMBUKUMBU YA MIAKA 22 YA KIFO CHA DR. FRANCIS MW. MSELLEMU

                                        DR. FRANCIS MW. MSELLEMU 1941- 1996 

 Baba, Ni Miaka 22 sasa tangu uondoke hata bila ya kutuambia neno la KWAHERI! Maisha yetu hayajawahi kuwa rahisi bila uwepo wako, Baba. Japo watu wanatuona tukicheka , hawajui ni kiasi gani mioyo yetu inahuzunika kwa kukukosa malezi, mapenzi na uwepo wako wewe. Hata hivyo tunamshukuru MUNGU kwa kuendelea kutulinda, kututunza na kutubariki. Ameedelea kuwa kweli kwetu Mume wa Mjane na Baba wa Yatima.

 Tunakuombea Pumziko la Milele, na tukiamini kwamba siku moja tutakutana na tutaimba Halleluya pamoja na wewe mbinguni. Unakumbukwa daima na Mke wako Mpendwa Kodawa Mikaline Msellemu - ‘Mama K’ kama ulivyo kuwa umezoea kumuita, Watoto, Wakwe zako, pamoja na Wajukuu. Ndugu , Jamaa na Marafiki nao hawajakusahau. ‘Mamillioni Wanaitegemea’-Pumzika kwa Amani DAD!

April 24, 2018

JE UNAFAHAMU KWAMBA UNAWEZA KUPENDEZESHA NYUMBA YAKO NA JUMIA?

Na Jumia Tanzania


Asilimia kubwa miongoni mwetu tunaishi kwenye nyumba ambazo hatuwezi kupaita ni nyumbani. Najua unaweza ukajiuliza kuna tofauti gani kati ya nyumba na nyumbani.

Nyumba ni jengo ambalo unaishi na kukupatia mahitaji yako ya msingi pamoja na hali ya usalama. Wakati, nyumbani ni mahali ambapo panakupatia amani na utulivu wa kiakili, mahali ambapo unatamani kuwepo pindi unapokuwa mbali na pilikapilika za ulimwengu.


Lakini jambo la kusikitisha miongoni mwa watu wengi wanaishi katika nyumba ambazo hazistahili kuziita ni nyumbani. Mwonekano wao nje na shughuli wanazozifanya ni tofauti kabisa na mahali wanapoishi na kutumia muda mwingi kutafakari mustakabali wa maisha yao ya kila siku.

Je na wewe unadhani kwamba nyumba yako unaweza kuiita ni nyumbani? Unajisikia vibaya kwamba sehemu unayoishi haistahili kuitwa nyumbani? USIJALI


Amini usiamini nyumba yako inaweza kuwa na muonekano mzuri, wa kisasa na wenye kustarehesha bila ya kutumia gharama kubwa! Jambo la msingi ni kufahamu ni kwa namna gani unaweza kufanya manunuzi ya vifaa ambavyo vitaipendezesha nyumba yako au sehemu unayoishi!

Jumia, inaendesha kampeni inayokwenda kwa jina la ‘BIG HOME MAKEOVER.’ Kampeni hii imedhamiria kuwawezesha wateja wake na watanzania kwa ujumla kuwa na nyumba zenye hadhi ya kuitwa nyumbani. Kupitia kampeni hii Jumia inalenga kupendezesha nyumba za wateja wake kwa kuwapatia mapunguzo makubwa ya bei ya vifaa mbalimbali vya nyumbani.


Akizungumzia juu ya kampeni hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa na Vifaa vya Nyumbani wa Jumia Tanzania, Priscilla Eliphas ameelezea kuwa, “tumegundua kuwa watu wengi wana kasumba ya kutumia vifaa vya nyumbani kwao kwa muda mrefu. Kwa mfano, unaweza kukuta mtu anatumia jokofu (friji), jiko la umeme, mashine ya kufulia nguo au kupasha chakula moto pamoja na samani za ndani kwa muda wa takribani miaka 10! Na unaweza kustaajabu ni sababu zipi zinazopelekea mtu kuendelea kutumia vifaa kwa muda mrefu kiasi hiko! Na bado wengi miongoni mwao huendelea kuvitumia kadri iwezekanavyo. Tunafahamu kwamba vifaa kama hivyo ni uwekezaji mkubwa unaofanywa kwenye nyumba za kuishi hivyo ni dhahiri kwamba watu huwa makini kwenye ubora na makampuni yanayotengeneza hivo vifaa.” 

“Jumia inafahamu kwamba kufanya mabadiliko kwenye nyumba hususani kuifanya iwe na muonekano mpya na wa kuvutia ni kazi kubwa na tena yenye gharama. Hiyo ndiyo sababu kubwa iliyotupelekea kuja na kampeni ya kupendezesha nyumba za wateja wetu. Kwa kuliona hilo tumekuja na kampeni ya zaidi ya wiki moja ya manunuzi ya vifaa tofauti vya nyumbani kama vile jikoni, sebuleni na mapambo ya nyumbani. Kampeni hii imeanza tangu Aprili 16 na kudumu mpaka Aprili 26, wateja wataweza kununua bidhaa lukuki za nyumbani kwa bei nafuu zenye ofa na mapunguzo makubwa,” alihitimisha.


Jumia inawasihi wateja wake kuitumia kampeni hii ipasavyo kwani wameshirikiana na kampuni kubwa za nchini Tanzania na kimataifa zinazotengeneza bidhaa zenye ubora wa kuaminika kama vile Samsung, Bruhm, Sony, Geepas, Nippotec, TCL, Star X, Philips, Aborder, Nikai, Ocean na Tronic. Cha kuvutia zaidi kuna mapunguzo ya bei, ofa, vocha za bure na zawadi kemkem kupitia kwenye tovuti yao! 

Wateja wanaweza kufanya manunuzi kwa urahisi kupitia mtandaoni, mahali popote walipo kwa bei za kipekee. Kwa kuongezea, bidhaa hufikishwa kwa mteja alipo kwa uharaka zaidi huku mteja akiwa na fursa ya kufanya malipo baada ya kuridhika na bidhaa alizoziagiza. Wateja wamepewa machaguo mengi zaidi ya bidhaa, takribani bidhaa zaidi ya 20,000 zimewekwa mtandaoni huku punguzo la bei likifika mpaka asilimia 60! 

TCRA YASISITIZA MATUMIZI SAHIHI NA SALAMA YA MITANDO NCHINI

Katika kupambana na makosa ya uhalifu wa kimtandao nchini TCRA kwa kushirikiana na kampuni ya Kingdom Heritage ilifanya semina kwa vijana yenye lengo la kuwajengea uelewa wa namna nzuri ya matumizi na usalama Mtandao.

Semina hiyo ilifanyika mwishoni mwaka wiki iliyopita katika ukumbi wa Buni Hub tume ya Sayansi Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na vijana kutoka vyuo na taasisi mbalimbali za serikali na binafsi.

Mwanansheria mwandamizi kutoka TCRA, Dk Philip Filikunjombe alipokuwa akizungumza katika warsha hiyo alisema  kulingana na ukuaji wa miundombinu ya TEHAMA inakuwa kwa kasi na kusababisha matokeo chanya na hasi katika jamii zetu
“Katika majira haya ya maendeleo ya TEHAMA waharifu wanatumia mwanya huo kufanya uharifu katika mifumo mbali mbalimbali ya Kompyuta hivyo tunatakakiwa kuwa makini kwa watumiaji wa mitandao na wadau wa TEHAMA nchini,” alisema Dk Filikunjombe.

Alisema kama TCRA wanazidi kusisitiza kuhusu matumizi sahihi na salama ya mitandao tena yenye maadili ili kupunguza uhalifu huo, Kwa kushirikiana na Jeshi la polisi kitengo cha uhalifu wa kimtandao.

Mwanzilishi wa Jamii Forums na muwasilishaji mada katika warsha hiyo, Maxence Melo alizungumzia fursa mbalimbali zinazopatikana katika mitandao na miundombinu ya TEHAMA kwa kuwasihi vijana waliokuwa hapo kuwa wabunifu katika majira haya na kuja na mifumo suluhisho itakayoweza kutumika katika jamii zetu.

“Serikali pia kupitia wizara au mamlaka zinazohusika kusapoti juhudi za vijana wabunifu katika TEHAMA  kwa miundombinu na kanuni na taratibu rafiki ili waweze kujifanikisha katika ubunifu wao mpaka kijipatia kipato binafsi na tafa zima kwa ujumla.” Alisema Melo.

Mtaalamu wa masuala ya ulinzi katika mfumo ya Kompyuta na TEHAMA nchini kutoka Kampuni ya Kabolik, Robert Matafu alizungumzia  namna ya kujilinda dhidi ya mashambulizi ya kimtandao na kuwa salama mtandaoni.

“Nchi nyingi za Afrika tunakosa uelewa wa maarifa ya kujilinda na mashambulizi ya kimtandao na kupelekea kupata hasara sana katika taasisi au watu binafsi kutokana na mashambulizi hayo,” alisema Matafu.

Aliongeza “Takwimu zinaonyesha taasisi nyingi afrika na Tanzania tukiwepo hatuwekezi vya kutosha katika mifumo ya kiulinzi na usalama mtandao,kwa kufanya hivyo tunaongeza asilimia kubwa za kupata mashambulizi ya kimtandao katika tasisi zetu,” alisema.

Awali, Mkurugenzi wa Kampuni ya Kingdom Heritage waandaaji wa semina hiyo Tunu  Bashemela alisema wao kwa sehemu yao wanaunga mkono juhudi za serikali kupitia TCRA katika kupambana na makosa ya uharifu wa kimtandao kwa kutoa elimu kwa umma hasa vijana ambao ndio rika linalotumia sana mitandao.

“Ili kujua matumizi sahihi na salama vijana mliopo hapa lazima mtambue kuwa sheria ya makosa ya uhalifu wa kimtandao ipo na inafanya kazi lazima tuheshimu na kutii vitu inavyotuzuia kufanya bali tutumie mitandao kwa namna za ubunifu zenye kutuletea fedha na kujiingizia kipato,” alisema Bashemela.Mwanansheria mwandamizi kutoka TCRA, Dk Philip Filikunjombe

Mwanzilishi wa Jamii Forums mmoja kati ya wawasilishaji mada katika warsha hiyo, Maxence Melo
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kingdom Heritage ambao ndio waandaaji wa semina hiyo Tunu  Bashemela
Vijana na mbalimbali watumiaji wa mitandao na wadau wa TEHAMA walioudhulia semina hiyo wakifuatilia kwa makini


Mtaalamu na Mshauri wa masuala ya ulinzi katika mfumo ya kompyuta na TEHAMA nchini kutoka Kampuni ya Kabolik, Robert Matafu katika mjadala na nini kifanyike ili kupunguza na kukomesha matukio ya uhalifu wa mtandao nchini.
  Mtendaji Mkuu wa tzNIC  Abibu Ntahigiye katika mjadala wa katika mjadala na nini kifanyike ili kupunguza na kukomesha matukio ya uhalifu wa mtandao nchini.
Mwanzilishi wa Jamii Forums katika mjadala na nini kifanyike ili kupunguza na kukomesha matukio ya uhalifu wa mtandao nchini.

RAIS MAGUFULI AUFAGILIA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF KWA UWEKEZAJI WENYE TIJA DODOMA

 Rais wa Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli mwenye mkasi), akiungana na baadhi ya mawaziri na viongozi wengine kukata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa jingo la kitegauchumi la Mfuko wa Pensheni wa PSPF, (PSPF DODOMA PLAZA), mjini humo Aprili 23, 2018. Jengo hilo lenye urefu wa ghorofa 12, tayari limepangishwa kwa takriban asilimia 100.
 Rais Magufuli, akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, mara baada ya kufunua kitambaa ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa jingo la kitega uchumi la Mfuko huo mjini Dodoma.


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Dodoma


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, amefurahishwa na uwekezaji uliofanywa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF wa kujenga jingo la kitegauchumi mkoani Dodoma.


Kilichomfanya Rais Magufuli kufurahishwa na uwekezaji huo ni kuona jengo hilo lenye ghorofa 12 tayari limepangishwa kwa asilimia 100 hata kabla ya uzinduzi rasmi uliofanyika Aprili 23, 2018.
“Ninyi mmemaliza tu tayari asilimia 100, mliangalia kwamba Dodoma ni makao makuu na mahitaji ya nahitajika kwa ajili ya majengo, hongereni sana kwa kupanga mikakati yenu vizuri kisayansi.” Alisema Dkt. Magufuli na kutoa hakikisho, “Pamoja na kuunganishwa kwa Mifuko hii ya Hifadhi ya Jamii ninyi wafanyakazi wa PSPF mjihesabu kuwa hamtapoteza nafazi zenu, lakini pia jengo hili limeboresha na kupendezesha mandhari ya Dodoma ambako ni makao makuu ya nchi yetu.” Alisema Rais Magufuli wakati akihutubia kwenye uzinduzi wa jengo hilo uliokwenda sambamba na ufunguzi rasmi wa makao makuu ya NMB Bank (Kambarage) ambao ni miongoni mwa wapangaji wakubwa kwenye jingo hilo lililoko barabara ya kuelekea chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Rais pia alifurahishwa na ushiriki wa watanzania katika ujenzi wa jengo hilo.
“Nimefurahi kusikia kuwa jingo hili limesanifiwa na ujenzi wake kusanifiwa na watanzania, ma contractors na consultants na kwamba takriban watanzania 250 walipata ajira wakati wa ujenzi.” Alipongeza.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, alisema, PSPF ndio Mfuko wa kwanza wa Hifadhi ya Jamii kuweka kitegauchumi cha jingo mkoani Dodoma na hivyo kuisaidia serikali ya awamu ya tano katika azma yake ya kuhamia makao makuu ya Nchi, mjini Dodoma.
Aidha Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu,
akielezea historia ya uwekezaji huo alisema, Mfuko ulipewa viwanja vya mradi huu na iliyokuwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) mwaka 2012 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kuendeshea shughuli za Mfuko pindi inapotokea dharura (business continuity) pamoja na kibiashara. Kazi ya usanifu na ujenzi wa jengo hili lilianza Julai 2015 na kukamilika Januari 2018 na kwa sasa jengo liko kwenye kipindi cha uangalizi (Defect Liability Period) ambacho kitaisha Januari 2019. Gharama tarajiwa za mradi yaani “contract sum” ni shilingi bilioni 37.02. Mpaka sasa Mfuko umeshalipa kiasi cha Shilingi za Kitanzania bilioni 30.56.
Jengo hili lina minara miwili, mmoja ukiwa na ghorofa 11 na mwingine ukiwa na ghorofa 3. Ukubwa wa jengo ni mita za mraba 15,741.60 pamoja na eneo la maegesho kwa ajili ya magari 161. Matumizi ya jengo ni kwaajili ya ofisi na shughuli za kibiashara.
“Hadi sasa jengo limepata wapangaji ambao kwa uchache ni kama ifuatavyo; NMB Bank, AZANIA Bank, TIB Corporate Bank, Benki ya Kilimo, GIZ, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), TASAF, TANAPA, TBS, Gaming Board, PPRA, Makao Makuu ya TARURA, Wizara ya Mambo ya Ndani, Sekretarieti ya Maadili ya Watumishi wa Umma, Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), ambao hawa pamoja na wengine wanafanya jengo kuwa limepangishwa kwa asilimia 98. Na kufikia leo Mfuko umeshakusanya kiasi cha Shilingi za Kitanzania 1.06 bilioni kutokana na malipo ya  pango na tunatarajia kukusanya kiasi cha Shilingi bilioni 4.7 kwa mwaka na kufikia miaka minane mradi utakua umerejesha fedha zote zilizowekezwa.”Alibainisha Bw. Mayingu.

 Rais akitoa hotuba yake.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PSPF, Mhandisi Musa Iyombe, akitoa hotuba yake.
 Bw. Mayingu akitoa hotuba yake.
 Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Bernard Kibese, (kulia), akibadilishana mawazo na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Venance Mabeyo, (wakwanza kushoto), na Mkuu wa Jeshi la Polisi, (IGP), Simon Siro, wakati wa uzinduzi huo.
 Wakurugenzi wa PSPF
 Mameneja wa PSPF
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Binilith Mahenge, (kushoto), akipokewa na Afisa Mwandamizi wa Uhusiano wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi wakati akiwasili kwenye eneo la tukio.
 Rais, baadhi ya mawaziri na viongozi wengine, wakiwa katika picha ya pamoja na Bodi ya wadhamini na wafanyakazi wa PSPF.
 Hili ndio jingo la PSPF DODOMA PLAZA lenye ghorofa 12 lililozinduliwa na Rais John Magufuli mjini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, akitoa hotuba yake.
 Baadhi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri, kutoka kushoto, Mhe. Luhaga Mpina (Waziri wa Mifugo na Uvuvi), Mhe.Juliana Shonza, (Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo), Mhe. Profesa Joyce Ndalichako, (Waziri wa Elimu) na Mhe.Jumaa Aweso, (Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji).
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, (kulia), akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, mwishoni mwa hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani wa PSPF, Bi.Costantina Martin, (kushoto), akibadilishana mawazo na Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo, Dkt. Hassan Abass, (katikati) na Afisa Mwandamizi wa Uhusiano wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi.
Kikundi cha Sanaa kikitumbuiza kwenye hafla hiyo.

April 23, 2018

Airtel kuviwezesha vikundi vya kinamama kujiendesha kidigitali


Diwani wa Kata ya Kibirizi Manispaa ya Kigoma Mjini Yunussa Rashid akikata utepe kuzindua duka la kisasa la kampuni za simu za mkononi ya Airtel Tanzania ambalo limefunguliwa mjini Kigoma juzi kwa lengo kurahishisha wateja wa kampuni hiyo kupata huduma kwa karibu zaidi.
XXXXXXXXXXXXX
·  Zaidi ya vikundi vya wajasiriamali 100 kunufaika na huduma ya Timiza Vikoba na Mafunzo ya Tehama

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imewahasa vikundi vya kina mama wajasiriamali kutumia fursa wanazozitoa kupitia bidhaa na huduma mbalimbali za kibunifu ikiwemo Timiza Vikoba ili kujiendesha kidigital na kukuza biashara zao. Hayo yalisemwa na meneja miradi wa Airtel Bi Jane Matinde wakati wa mkutano wa viongozi wa vikundi vya kina mama wajasiriamali jijini Dar uliondaliwa na Star Women group.

Akitoa ufafanuzi wa kina  Matinde alisema “Timiza vikoba ni huduma inayowawezesha vikundi kuweka na kuchukua mikopo kupitia simu zao za mkononi kwa kupitia huduma ya Airtel Money, huduma inayotolewa na Airtel kwa kushirikiana na benki ya Maendeleo.

Timiza Vikoba inaviwezesha vikundi vya kuanzia watu 5 hadi 50  kujisaji na  kufungua akaunti ili kufaidika na huduma ya kutuma michango yao ya kila wiki, kuomba mikopo na kufanya marejesho ya mikopo wakiwa nyumbani au mahali popote pale kwa usalama na urahisi zaidi masaa 24 siku saba za wiki kwa gharama nafuu”.

Matinde aliwashauri wanawake hao wajarisiamali kutumia njia za teknologia ya kisasa katika kufanya miamala ya kifedha kwa usalama,  uhakika na urahisi zaidi kupitia huduma ya Timiza Vikoba “ huduma hii  itawarahisishia sana kutuma pesa za michango na marejesho kupitia simu, itaokoa muda wa kukutana na kuweka uwazi kwani kila mwana kikundi anapoweka pesa fedha au kuomba mkopo kila moja anapata taarifa hapohapo nakuridhia, nawahimiza mchangamkie fursa hii.

Pamoja na huduma ya Timiza pia tunawawezesha kupata mafunzo ya Tehama kupitia maabara ya kompyuta ya Airtel fursa iliyopo katika shule ya msingi Kijitonyama. Tayari tunao wajasiriamali ambao wanaendelea kunufaika na masomo haya hivvo hii pia ni fursa kwenu kujitokeza na kujiandikisha kwa wingi. Mafunzo haya ya Tehama yatawawezesha kutunza rekodi na mahesabu ya biashara  vizuri zaidi, kutumia aplikesheni mbalimbali kuendesha biashara zenu kwa ufanusi na  kukuza mitaji alisisitiza Matinde

Kwa upande wake Mwanzilishi wa Star Women group na mwandaji wa mkutano huo, Bi Queen Cuthbert Sendiga aliwashukuru sana Airtel kwa kuwapatia wakinamama hao wajasiriamali fursa kupitia huduma na bidhaa zao na kuwaomba  waendelea kushirikiana nao katika kutoa fursa hizi zitakazowainua wakina mama kwani ndio muhimili wa familia na kichochoe kikubwa katika kukuza uchumi wa jamii na nchi kwa ujumla. Aidha aliahidi kuwahamasisha kina mama wengi kujiunga na masomo ya Tehama kwani uelewa bado ni Mdogo na pia kutumia technologia ya kisasa katika kuweka na kukopa kupitia huduma ya Timiza Vikoba.

Tangu kuzinduliwa kwa huduma ya Timiza Vikoba wachama zaidi ya 261,673 na vikundi 26,158 vimeshajiandikisha huku mikopo zaidi ya 774 yenye thamani ya shilingi milioni 49 kutolewa kwa vikundi hivyo.

COCA-COLA BONITE YAMWAGA ZAWADI KWA WASHINDI WA PROMOSHENI YA 'MZUKA WA SOKA NA COKA'

 Mmoja wa washindi wa pokipiki akikabidhiwa zawadi yake.
 Baadhi ya washindi wa luninga katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa zawadi zao
Washindi wa pikipiki wakijaribu kuendesha pikipiki zao baada ya kukabidhiwa wakiwa na Meneja Mauzo wa Bonite, Boniface Mwassi.
Wshindi wa fedha taslimu shilingi 100,000/-baada ya kukaidhiwa zawadi zao na Afisa Mwandamizi wa Mauzo wa Bonite, Godfrey Imani.
Baadhi ya washindi wakisubiri kukabidhiwa zawadi zao.

April 20, 2018

TUCTA MEI MOSI 2018 IRINGA ; HII NI HESHIMA KUBWA KWA MKOA WA IRINGA RC MASENZA

Mkuu  wa mkoa wa  Iringa  Amina  Juma Masenza


Rais wa shirikisho la vyama huru vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Tumaini Vyamhokya katikati akiongoza kuimba wimbo wa wafanyakazi wakati wa kikao na  wanahabari mjini  Iringa .
..................................................................................................................................................
Na  MatukiodaimaBlog

WAKATI  maadhimisho ya  siku  ya  wafanyakazi duniani  kwa  nchini  Tanzania  yaliyoandaliwa na  shirikisho la vyama huru vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) yakitaraji  kufanyika  mkoani  Iringa   kitaifa  mkuu   wa mkoa  wa Iringa  Amina  Masenza  amesema  mkoa  wa Iringa  kuwa  mwenyeji wa  mei  mosi ni  heshima  kubwa katika  Taifa .

 Akizungumza  na  wanahabari  leo  ofisini kwake    kuhusiana na maandalizi ya  Mei  Mosi  Kitaifa  alisema  kuwa  mkoa  wa  Iringa  umeteuliwa  kuwa mwenyeji  wa maadhimisho hayo  ambapo  mgeni  rasmi atakuwa  ni  Rais  Dkt  John Magufuli .

Alisema  kuwa katika  maadhimisho hayo ya  Mei  Mosi  kitaifa  kauli   mbiu  ni Kuunganishwa kwa  mifuko ya hifadhi ya  jamii kulenge  kuboresha mafao ya  wafanyakazi  na  kuwa  kupitia maadhimisho hayo wakazi  wa  mkoa wa  Iringa na  wafanyabiashara  watapata   fursa  kubwa  ya  kujitangaza  pamoja na  kuonyesha shughuli  zao.
Mkuu  wa mkoa wa  Iringa  Amina  Juma  Masenza akila  kiapo  mbele ya  Rais  Dkt  Jonh  Magufuli  pindi  alipoteuliwa  kuwa mkuu wa mkoa wa Iringa

Katika maadhimisho hayo  ambayo   kilele  chake  kitafanyika  uwanja  wa Samora  mjini Iringa  kabla ya  kilele  kutakuwa na  michezo mbali  mbali  kama mpira wa miguu, kuvuta kamba ,bonanza la  michezo  tofauti  ,mpira wa pete ambayo yote yameanza toka  April  17 hadi  April  30 mwaka   huu .

Hata  hivyo  mkuu  huyo wa mkoa   wa Iringa mwenyeji wa  Mei  mosi kitaifa  mwaka  2018  Bi Amina Masenza alisema  sherehe  hizo zitahusisha  maonyesho  ya  shughuli ,huduma na  bidhaa mbali mbali  za wafanyakazi ,taasisi  za  umma na  binafsi ,wawekezaji  na wajasiliamali  zitakazofanyika  uwanja  wa Kichangani  Kihesa  mjini  hapa .

Hata  hivyo  alisema  kwa ajili ya  kuufanya mkoa wa Iringa  uzidi  kuwa fursa kwa  wageni  kutembelea  vivutio  vya  utalii kama  hifadhi ya  Ruaha  na vingine   serikali  imekaa na  wafanyabiashara  wa  nyumba  za  kulala wageni na  Hoteli  ili  kuepuka  kutumia mei  mosi  kupandisha   gharama  za  vyumba  kwa wageni .


Bi  Masenza  amewataka   wananchi wa  mkoa  wa  Iringa  na  wafanyakazi  wote   kujitokeza kwa wingi  kumlaki Rais  wetu mpendwa  wetu Dkt  John  Magufuli .