Tangazo

July 16, 2012

Mwandishi wa Habari Mwandamizi Chriss Mwambonda Amefariki Dunia

Marehemu Chriss Mwambonda (kushoto), enzi za uhai wake akipokea cheti kutoka kwa Mkurugenzi wa Michezo Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Leonard Thadeo katika moja ya shughuli za kimichezo.
 *****************
 Mwandishi wa Habari Mwandamizi Criss Mwambonda amefariki dunia usiku wa kuamkia jana Julai 15.

Taarifa kutoka kwa ndugu yake aitwaye Obi pamoja na rafiki yake wa karibu Jimmy Chika ni kwamba taratibu za mazishi zinafanywa nyumbani kwao Mbezi, Dar es Salaam.

Mambo mengine kuhusiana na jambo hili tutajulishana wadau. Ni msiba wa wote na sote njia yetu ni moja.

Tumuombee Mwenyezi Mungu amuweke mahala pema peponi, marehemu Mwambonda ambaye amefanya kazi vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini.

No comments: