Tangazo

July 16, 2012

MUKAMA AKUTANA NA MWEKEZAJI KUTOKA NIGERIA

Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama akimkaribisha kwa bashasha, Mwekezaji kutoka Nigeria, Aliko Dangote, wa Dangote Industries Ltd alipowasili Ofisi Ndogo ya Makamo Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba Jijini Dar es Salaam,  Julai 15, 2012, kwa ajili ya mazungumzo mbalimbali ikiwemo namna mwekezaji huyo anavyoweza kufanyakazi na Chama Cha Mapinduzi katika nyanja kadhaa za kibiashara. Katikati ni Balozi wa Nigeria hapa nchini, Dk. Ishaya Nanjabu. (Picha na Bashir Nkoromo).

Mukama na Ujumbe wa mgeni huyo wakiwa katika mazungumzo kwenye ukumbi wa sektretarieti Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM.

Mukama na Ujumbe  wake wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni huyo na Ujumbe wake, mbele ya Ofisi Ndogo ya Makamo Makuu ya CCM, kwenye jengo ilimozaliwa TANU.

No comments: