Tangazo

October 31, 2011

NBC Yapiga jeki ujenzi wa jengo la maabara la DUCE

Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, Robi Matiko-Simba (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi ya shs milioni 10 kwa Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Prof.  Salome Misana zilizotolewa na benki hiyo kusaidia ujenzi wa jengo la maabara la Shule ya Sekondari Chang’ombe inayomilikiwa na DUCE. Hafla ya makabidhiano ilifanyika chuoni hapo Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katikati ni Mshauri wa Mambo ya Habari wa NBC, Redemptus Masanja (wa pili kushoto) na Naibu Mkuu wa Chuo Utawala, Prof. Bavo Nyichomba.

Mshauri wa Mambo ya Habari wa NBC, Redemptus Masanja (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi ya shs milioni 10 kwa Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Prof.  Salome Misana zilizotolewa na benki hiyo kusaidia ujenzi wa jengo la maabara la Shule ya Sekondari Chang’ombe inayomilikiwa na DUCE. Hafla ya makabidhiano ilifanyika chuoni hapo Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katikati ni Meneja Mahusiano wa NBC, Robi Matiko-Simba (wa pili kushoto)  na Naibu Mkuu wa Chuo Utawala, Prof. Bavo Nyichomba.
                                 *************************************************

NA MWANDISHI WETU
BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC), imekabidhi hundi ya shs milioni 10 kuchangia ujenzi wa jengo la maabara ya Shule ya Sekondari Chango’ombe inayomilikiwa na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE).

Akikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa chuo hicho, Prof. Salome Misana, Meneja Mahusiano wa NBC, Robi Matiko-Simba alisema msaada huo ni sehemu ya majukumu ya benki hiyo ndani ya mfuko wake wa kuisaidia jamii (CSR)

“ Kama NBC suala la elimu ni muhimu mno hususani kusaidia chuo kama DUCE kwani ubora wa elimu atakayopata mwalimu kwa sasa, mchango wake ni mkubwa sana katika ubora wa elimu watakayopata watoto watakaofundishwa na walimu hao,” alisema Bi. Robi.

Alisema ni kwa kuzingatia hilo hadi sasa Benki yas NBC imeshatumia zaidi ya shs bilioni 1.5 katika masuala ya elimu ikisaidia katiukia maeneo mbalimbali kama vile ujenzi wa madarasa, ununuaji wa madawati, vitabu, madaftari na vifaa vingine vya kufundishia.

Akipokea msaada huo Mkuu huyo wa DUCE, Prof. Salome Misana aliishukuru Benki ya NBC kwa kuunga mkono juhudi za chuo hicho katika kuboresha miundo mbinu ya chuo hicho katika jitihada zake za kuboresha masomo ya sayansi katika chuo hicho kilichoanzishwa mwaka 2005 ikiwa ni juhudi za serikali katika kupambana na tatizo la uhaba wa walimu na wataalamu wengine katika sekta ya elimu.

Alisema katika kuadhimisha miaka 50 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sambamba na miaka 50 ya Uhuru, DUCE pamoja na mambo mengine kiliazimia kuanzisha mchakato wa ujenzi wa jengo la maabara ya Shule yao ya Sekondari Chang’ombe wakiwa na kauli mbiu ya ‘Tuinue Sayansi na Teknolojia Mashuleni na Vyuoni kaka Chachu ya Maendeleo ya Kiuchumi Tanzania’.

Mkuu huyo wa DUCE alisema mchakato huo ulizinduliwa na rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Mohammed Gharib Bilal Septemba 13 huku makadirio ya ujenzi huo ukitegemewa kugharimu wastani wa shs bilioni 2.

Naye Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Bavo Nyichoma alisema mchango wa NBC ni muhimu sana katika jitihada zao za kuhakikisha ujenzi wa maabara ya shule hiyo zinafanikiwa kwani sanyansi ndio gurudumu la maendeleo.

“Nchi zote zilizoendelea ni kutokana na matunda ya wanasayansi wake na hata sisi ili tuweze kupata wanafunzi wazuri ni lazima tuwekeze kwa vitendo katika elimu ya sayansi,” alisema.

Chuo Kikuu cha DUCE kikiwa na wanafunzi 616 kati yao 382 wakichukua masomno ya sayansi hutumia Shule ya Sekondari Chang’ombe kama sehemu ya kufanya mazoezi ya ufundishaji kwa vitendo.  



No comments: