Tangazo

November 7, 2011

AIRTEL TANZANIA NA LEAF TOBACCO ZAPANDA MITI TANGA UZINDUZI WA MICHEZO YA SHIMIWI

Makamu mwenyekiti wa SHIMIWI, Daniel Mwalusamba akipanda mti katika shule ya sekondari ya Ufundi Tanga, Kushoto ni Mtaalam wa Miti wa TLT, Hamisi Mbonga akifukia shimo na (kulia) ni  Afisa Mazingira wa Airtel, Mkama Manyama akimwagilia mche.  Miti hiyo imepandwa na kampuni ya simu za mkononi Airtel ikishirikiana na kampuni ya Tumbaku (TLT) wakati wa uzinduzi wa michezo ya SHIMIWI mwishoni mwa wiki.

Washiriki wa Mashindano ya michezo ya SHIMIWI  2011 wakipanda miti katika shule ya sekondari ya Ufundi Tanga wakati wa ufunguzi  wa michezo  hiyo  inayofanyika mwaka huu Mkoani Tanga ambapo kampuni ya  simu za mkononi ya Airtel  imedhamini michezo hiyo na kushirikiana na kampuni ya Tumbaku Tanzania (TLT) katika zoezi zima la kupanda miti.  
                                         ******************************************
·  Michezo itakayoshindaniwa ni Soka, Netiboli, Bao, Karata, Kuvuta Kamba na Drafti.
 
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel ikishirikiana na kampuni ya Tobaco TLT mwishoni mwa wiki imejumuika na mamia ya wananchi waliohudhuria michezo ya SHIMIWI  inayofanyika katika mkoa wa Tanga katika zoezi la kupanda miti  katika shule za sekondari za Galanosi na Ufundi.

Zoezi hili la kupanda miti limefanya katika uzinduzi wa michezo hii inayaofanyika mkoani Tanga kwa muda wa wiki mbili kwa kupanda miti elfu tatu.

Halfa hii imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali ikiwamo Mgeni Ramsi mkuu wa mkoa wa Tanga Kanali Mstaafu Chiku Galawa pamoja na  mkuu wa wilaya ya Tanga Ibrahim Hassan Hussein ambapo nao walishiriki katika upandaji wa miti hiyo.
 
Wakizungumza kwa katika shughuli hii ya upandaji miti, Mkuu wa  mkoa wa Tanga  Luteni Kanali mstaafu Chiku  Galawa aliwashukuru kampuni ya Airtel na TLT kwa kupanda miti mkoani Tanga na kuwashukuru waandaaji wa michezo ya  SHIMIWI kwa kuleta michezo hiyo mkoani hapo ambapo kwa muda wa wiki mbili shughuli za biashara zitaongezeka na kuinua pato la wakazi mkoani Tanga.

Pia aliwaasa walimu na wanafunzi wa shule za sekondari hizo kutunza mazingira na kuitunza miti iliyopandwa leo na kuhakikisha inastawi na kukuwa kama inavyotarajiwa.
Afisa mazingira wa Airtel bwana Mkama Manyama alisema “leo tunayo furaha kujumuhika na  wenzetu shimiwi pamoja na kampuni ya Tobacco TLT katika zoezi la kupanda miti ambalo linaweka historia ya pekee katika shimiwi mwaka huu wa 2011 hapa mkoani Tanga . Sisi Airtel tunachukua nafasi hii kushiriki kikamilifu katika uhifadhi wa mazingira na kutunza rasilimali asili ambazo zitasaidia hadi kizazi  kijacho.

Kwa upande wake mwakilishi wa TLT bwana Fridoline Takisi aliongeza kwa kusema  Tanzania Leaf Tobacco  imekuwa mstari wa mbele katika kupanda miti kwenye mikoa mbalimbali nchini, hadi sasa TLT  kwa kushirikiana na wadau wake imepanda jumla ya miti zaidi ya 10,000 katika miji na mikoa mbalimbali nchini, hii ni katika kutimiza dhima yetu ya kutunza na kuhifadhi mazingira.

Mashindano ya Wizara, Idara na Mashirika ya Umma (SHIMIWI) yameanza rasmi mwishoni mwa wiki hii mkaoni Tanga na yatadumu kwa muda wa wiki mbili mfululizo huku zaidi ya TIMU 42 zikiwa zimethibitisha kushiriki
 
Katibu wa shirikisho hilo, RAMADHAN SULULU amesema”Sasa Mambo SHIMIWI yameiva,  Michezo itakayokuwepo katika mashindano haya ni SOKA, NETIBOLI, MCHEZO WA BAO, KUCHEZA KARATA, Kuvuta kamba na DRAFTI.

No comments: