Tangazo

February 7, 2012

BWANA GERALD KIMALI APATA 'JIKO'

Hayawi hayawi yamekuwa, Bwana harusi Gerald Kimali akiwa katika pozi la picha na mkewake Suzan Abias baada ya kufunga ndoa yao katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es Salaam Februari 4.2012, na kufuatiwana sherehe kubwa iliyofanyika katika ukumbi wa Brigedia Mess  Lugalo. Bwana harusi ni mfanyakazi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam  na Bibi harusi ni  Mwalimu wa Sekondari ya Bagamoyo.Picha/Albert Jackson

Bibi harusi Suzan Abias akiwa katika pozi wakati wa tafrija ya kumpongeza iliyofanyika katika ukumbi wa Brigedia Mess Lugalo.

Bwana harusi Gerald Kimali na mkewe Suzan Abias wakikata keki wakati wa tafrija ya harusi yao.  

Msanii aliyewahi kuwika na kikundi cha Kidedea, Clarence Abias akionyesha umahiri wa kupiga gita wakati alipokuwa akitumbuiza kwa kuimba wimbo wa 'Mtaa wa Saba', wakati wa tafrija ya kumpogeza  dada yake  Suzan Abias ambaye alifunga ndoa na Gerald Kimali.


UTANIPENDA TU ; Bwanaharusi Gerald Kimali akimpigia gita mkewe Suzan Abias wakati alipokuwa akimwimbia wimbo wa sasa umehamia mtaa wa saba  wakati alipokuwa wakifungua muziki katika  sherehe yao.

STAIRI ZA PICHA HIZO .Bwanaharusi Gerald Kimali na wapambe wao wakiwa wamembeba bibi harusi Suzan Abias wakati wa kupiga picha.


No comments: