Tangazo

February 2, 2012

Serengeti Breweries Limited (SBL) Moshi yatoa Tamko juu ya matumizi ya maji

Kufuatia tuhuma zinazotolewa, Bodi ya Wakurugenzi na Uongozi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, inapenda kutoa tamko rasmi kuwa  Kiwanda cha Bia cha Serengeti cha mkoani Moshi hakitumii maji kutoka mamlaka ya maji safi na maji taka ya Moshi (MUWSA) Kiwanda cha Moshi kina visima viwili ambavyo vinatosha kwa ajili ya matumizi ya kiwanda.

Tunafahamu na pia tunaguswa sana na uhaba wa maji unaoendelea katika Mkoa wa Moshi na tunaangalia jinsi tunaweza kufanya kazi pamoja na idara husika ili tuweze kuwa sehemu ya suluhisho la tatizo hili.

Kampuni ya Bia ya Serengeti inashiriki kikamilifu katika kuisaidia jamii , tuna mradi maalum wa maji “Water of Life” ambao lengo lake kuu ni kuwekeza kwenye miradi ya maji. Zaidi ya watu laki mbili wanafaidika na mradi wetu wa maji uliopo Mkuranga.

Kampuni pia imejenga hospitali kubwa na ya kisasa ya macho KCMC Moshi. Zaidi watu laki tatu kutoka Moshi na Afrika Mashariki watafaidika na mradi huu. Kituo hiki kimegharimu zaidi ya milioni 264.6 na kinasimamiwa na Kilimanjaro Christian Medical Center.

Imetolewa na
Idara ya Mahusiano na Mawasiliano ya Jamii.

No comments: