Tangazo

March 12, 2012

India Kuwekeza Zaidi Tanzania

By Pascal Mayalla      

India inajipanga kuwekeza zaidi nchini Tanzania, kufuatia mafanikio yaliyopatikana katika miradi mbalimbali ya ushirikiano kati ya India na Tanzania kuyonyesha mafanikio makubwa.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Balozi wa India nchini Tanzania, Bibi Hemalata Bhagirath, wakati alipotembelea mradi matrekta ya Kilimo Kwanza, unatekelezwa na shirika la SUMA JKT, eneo la Mwenge, jijini Dar es Salaam.

Bibi Bhagirathi amesema inchi yake, imeridhishwa sana na utekelezaji wa mradi huo, unaohusisha matrecta 1860 ya Farmtrack kutoka India kutokana na mkopo wa Dola Milioni 40 za Marekani, na matrecta hayo kukopeshwa kwa wakulima wa Tanzania, ili kufanya mapinduzi ya Kilimo kupitia mpango wa Kilimo Kwanza.

Balozi Bagirathi amesema, kufuatia mwitikio mzuri kwa Watanzania kwa matrekta hayo, nchi yake inaweza kuangalia uwezekano wa kufungua kiwanda cha matrekta hayo humu nchini ili kutosheleza kabisa mahitaji ya Kilimo Kwanza.

Mkurugenzi Mtendaji wa Suma JKT, Co. Ayoub Mwakang’ata, ameishukuru serikali ya India kuwezesha kupatikana kwa mkopo wa mradi huo na kusisitiza kuusimamia vizuri ili fedha za mkpo huo zirudi na faida.

Meneja Mradi, Col. Felix Semilano, amesema  baada ya serikali kuyapunguza bei matrekta hayo kutoka Shilingi Milioni 26 mpaka Shilingi Milioni 16, matrekta hayo sasa yanagombewa kama njugu.

Mkurugenzi wa Usharika TAMEKO, Mzee Remigius Mbawala, ameyasifu matrekta hayo, na kueleza yana uwezo mkubwa kwa sababu yametengenezwa mahsusi kwa ardhi na mazingira ya Tanzania.

No comments: