Tangazo

June 8, 2012

Balozi wa Uingereza afanya ziara Wizara ya Nishati na Madini

Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania, Bi. Diane Corner (kushoto) akisisitiza jambo kwenye kikao alichofanya na Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Profesa Sospeter Muhongo (katikati) mara baada ya kufanya ziara kwenye Wizara. Anayesikiliza upande wa  kulia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya madini, Mhe. Stephen  Maselle. Lengo la ziara yake ilikuwa ni kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Uingereza hususan katika sekta  za nishati na madini.

Waziri wa Nishati  na Madini Mhe. Profesa Sospeter Muhongo akimsikiliza kwa makini Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Bi. Diane Corner  katika kikao hicho. Kikao hicho kilihusisha  pia wataalamu wa  Wizara ya Nishati  na Madini.

No comments: