Luis Moreno Ocampo |
Arusha, Juni 8, 2012 (FH)
Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai, Luis Moreno Ocampo wiki hii alilihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juu ya hali ilivyo nchini Sudan na kulitaka kutafuta mbinu za kumkamata Rais Omar Al-Bashir na viongozi wengine nchini humo.
ICC
Ocampo ashinikiza kukamatwa kwa Al-Bashir: Mwendesha mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai, Jumanne wiki hii alilitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutafuta mbinu za kuwakamata viongozi nchiniSudan, akiwemo Rais Omar Al-Bashir.

Akilihutubia Barazahilo, Ocampo alisisitiza kuwa kitendo cha serikali ya Sudankukataa kumkamata Al-Bashir kunatoa changamoto ya moja kwa moja juu ya mamlaka lililonalo Barazahilo.
Rais Omar Al-Bashir. |
Siku moja kabla ya kulihutubia Baraza hilo, mwendesha mashitaka huyo aliongea na mkosanyiko huko New York, ambapo alipendekeza nchi zinazompokea Al-Bashir zinyimwe misaada, kamanjia mojawapo ya kushinikiza kukamatwa kwake.
Malawi Jumatatu ilitangaza kumkamata Rais huyo wa Sudan kama atahudhuria kikao cha wakuu wa nchi barani Afrika kitakachofanyika nchini humo mwezi ujao.
Mawakili wa Gbagbo waomba kusogezwa mbele kesi ya mteja wao: Mawakili wa aliyekuwa Rais wa Ivory Coast Laurent Gbagbo Alhamisi wiki hii waliiomba Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai kuahirisha hadi siku nyingine kikao cha kuchambuakamamakosa yanayomkabili mteja wao yanastahili kuthibitishwa. Awali, kikao hicho kilikuwa kimepangwa kufanyika Juni 18.
Mawakili hao walidai kuwa hali ya kiafya ya mteja wao imemfanya ashindwe kutoa mchango mahususi katika maadalizi ya kikao hicho. Mkuu huyo wa zamani wa nchi ambaye ni wa kwanza kushitakiwa katika mahakama hiyo alifikishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Disemba 5, mwaka jana ambapo alifahamishwa makosa yatakayomkabili ya uhalifu dhidi ya binadamu yanayodaiwa kutendeka chini mwake kati ya Disemba 16, 2010 na Aprili 12, mwaka jana.

No comments:
Post a Comment