Katibu wa TEF, Neville Meena |
JUKWAA la Wahariri (TEF), limeeleza kutokuwa na imani na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara na Katibu Mkuu wake Seth Kamuhanda kama wanaweza kufanikisha kupatikana kwa sheria ya vyombo vya habari kutokana na msuguano baina yao.
Taarifa iliyotolewa na TEF na kusainiwa na Katibu wake Neville Meena, inasema azimio hilo limetolea na wahariri watendaji wa vyombo vya umma, vinavyomilikiwa na mashirika ya dini pamoja na watu binafsi katika mkutano uliofanyika Morogoro kati ya Juni 3 mpaka 5 mwaka huu.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa, licha ya viongozi hao kualikwa kwenye mkutano huo ambao pamoja na mambo mengine ulijadili Mchakato wa Sheria ya Haki ya Kupata Habari na Huduma za Vyombo vya Habari nchini, ambao umekuwa ukisuasua kwa takriban miaka 10 sasa, hawakuhudhuria.
Inasema kuwa, vitu vingine muhimu vilivyokuwa vinajadiliwa ambavyo vilihitaji kiongozi kutoka wizarani kuwapo ni pamoja na kuwezesha kazi ya uandishi wa habari kufanyika kwa kuzingatia maadili, wajibu na weledi wa kitaaluma.
Mada nyingine ni kuimarisha weledi wa kitaaluma, uwajibikaji , utendaji wa kazi na uhuru wa vyombo vya habari na zaidi kujenga mfumo wa usimamizi wa maadili ndani ya vyombo vya habari.
“Kwa masikitiko makubwa, Waziri na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, hawakushiriki hata kwa kufungua mkutano huu kama walivyoombwa na Baraza la Habari Tanzania na wao wenyewe kuthibitisha kwa nyakati tofauti,” imesema sehemu ya taarifa hiyo na kuongeza:
“Tukio hili kwetu wahariri limetupunguzia imani kwa viongozi hawa, iwapo wataweza kutuvusha katika mabadiliko ya kitaaluma na yale ya kimfumo katika kukusanya na kutoa habari nchini,”.
“Kwa maana hiyo tumeazimia kwamba kwanza: Tunatoa taarifa rasmi ili umma wa Watanzania uweze kufahamu hali hii, lakini pili tutawasilisha rasmi malalamiko yetu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete aweze kuingilia kati hali hii kwa nia ya kuiokoa tasnia ya habari, ambayo ni muhimu kwa ustawi na afya ya taifa hili.”
Taarifa hiyo ilisisitiza kuwa, “Tunapenda kuwahakikishia Watanzania na Serikali kwa ujumla kuwa vyombo vya habari vimejizatiti na kujipanga kuwatumikia Watanzania kwa kuzingatia maadili na weledi wa hali ya juu pia kwa kuzingatia matakwa na maslahi ya umma.”
Ilisema kuwa, wanachoomba zana ya kutekeleza jambo hilo ambayo ni Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari na Sheria ya Haki ya Kupata Habari, ambazo mchakato wake umedumu kwa zaidi ya miaka 10 sasa bila kupatikana.
“Tunasema mikingamo inayokwamisha sheria hii imalizwe ili tuweze kupata sheria nzuri na kufanya kazi kwa uhuru na uhakika zaidi, hili la Waziri na Katibu Mkuu wizarani linaongeza wasiwasi wa kupatikana kwa sheria hizi.”
Ikifafanua mawasiliano yaliyokuwa yakiendelea kati ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) na wizara hiyo, ilisema kuwa walishatumia rasimu ya hotuba ambayo ilipaswa kusomwa kwanza na waziri ambaye ndiye alipaswa kuwa mgeni rasmi, kabla ya yeye mwenyewe (waziri) kutoa taarifa MCT kwamba, angewasilishwa na Katibu Mkuu wa Wizara, huku wakitoa udhuru kwamba walikuwa na kazi nyingine.
“Hatua ya viongozi hao kushindwa kufika katika mkutano huo muhimu kwa maendeleo ya tasnia ya habari nchini ikiwa ni pamoja na kushindwa kwao kutuma mwakilishi mwingine kutoka wizarani, si tu iliwashtua wahariri, bali iliwasononesha na kuwashangaza,”.
“Taarifa ambazo tulizipata zinaonyesha kuwapo kwa msuguano usio na afya kwa tasnia ya habari, kwa wizara na kwa serikali nzima kati ya Waziri na Katibu Mkuu. Kitendo cha wao kushindwa kutuma mwakilishi kutoka kwa viongozi na watendaji wengi waliojaa katika wizara hiyo ni ushahidi wa namna hali ilivyo mbaya na tete kimahusiano na kikazi katika wizara hiyo.”
Chanzo: Gazeti la Mwananchi Juni 08.2012

No comments:
Post a Comment