Tangazo

July 12, 2012

VODACOM KUWAPA WATEJA WAKE MARA TANO ZAIDI KWA KILA KIFURUSHI CHA INTERNETI

·        Wateja kuendelea kuperuzi Wikipedia, Facebook na Twitter bure
·        Ofa mpya kuwapa wateja wanaotumia intaneti huduma bora zaidi
 

Dar es Salaam Julai 12, 2012
 Wateja wa Kampuni ya Vodacom wana fursa nyengine murwa ya kufurahia mawasiliano kupitia njia ya intaneti ambapo sasa watapokea mara tano zaidi ya kila kifurushi cha data wanachonunua kupitia Vodacom kwa gharama nafuu.

Ofa hiyo inanuia kupanua wigo ya ofa zinazotololewa sokoni wakati huu kupitia kampeni maarufu ya Wajanja.

Ofa hii inaenda sambamba na ofa inayoendelea kwa wateja wa malipo kabla ambayo inawawezesha kuperuzi Wikipedia, Facebook na Twitter bure kila siku, ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha wateja wanafaidi zaidi na kubakia wakiwa wameunganishwa katika mitandao ya kijamii.

“Kila mmoja kuanzia wanafunzi, wafanyakazi, wafanyabishara na wengineo wana nafasi yake kutumia huduma za Intaneti kupata taarifa za masuala mbalimbali. Hivyo ni muhimu kuwapatia watu BURE huduma za kuperuzi kama vile Wikipedia hususan wanafunzi ili kuwawezesha kupata kwa haraka taarifa muhimu wanazozihitaji katika masomo,” amesema Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bw. Rene Meza

“Kwa kiasi kidogo cha Sh 250 kwa siku mteja wetu anapata 25MB ikiwa ni mara tano zaidi ya aliyokuwa akipata hapo awali ikimaanisha kwamba anaweza kuperuzi mtandao wa google na mengineyo kwa kasi zaidi na kuunganishwa na ndugu na marafiki,” ameongeza kusema Bw. Meza akidokeza kuwa kampeni ya Wajanja ambayo imehusisha pia matamasha ya burudani ya muziki sehemu mbalimbali ya nchi imekuwa na mafanikio makubwa na itazidi kubuni na kutoa ofa zaidi kumwezesha kila mmoja kutumia gharama nafuu katika mawasiliano.

Vifurushi vingine vinavyopatikana katika ofa hii ya pata tano zaidi ni 50MB kwa Sh 450 kwa siku, 150MB kwa Sh 2,500 kwa siku saba na 100MB  kwa Sh 2000 kwa matumizi ya siku thelathini.

Kujiunga na kununua vifurushi vya Intaneti za Vodacom ni rahisi. Mteja anahitajika kupiga *149*01# na kasha kuchagua aina ya huduma na kifurushi anachokihitaji.

No comments: