Tangazo

August 13, 2012

Kutoka Bungeni Leo

Mbunge wa jimbo la Mchinga ambaye pia ni Mwakilishi wa Bunge la Afrika Saidi Mtanda (kushoto) akisalimiana na Mbuge wa jimbo la Rungwe Magharibi,  Prof. David Mwakyusa (kulia) nje ya ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa Mwakilishi wa Bunge la Afrika. Katika uchaguzi huo mdogo Mtanda alimshinda mpinzani wake, Dkt. Hamis Kigwangalla kwa kura 145 kwa 72. Picha zote na Anna Nkinda wa MAELEZO

 Wananchi wakisubiri kuingia ndani ya ukumbi wa bunge  kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa nane, kikao cha 46  cha Bunge ambapo wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi iliwasilisha hotuba ya mapato na matumizi  kwa mwaka wa fedha 2012/2013.

Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa (kulia) akiongea jambo na  Mbunge wa Dole, Sylvester Mabumba (kushoto) nje ya ukumbi wa bunge  leo mjini Dodoma. Dk. Kawambwa amewasilisha leo  hotuba ya wizara hiyo ya mapato na matumizi  kwa mwaka wa fedha 2012/2013.


Baadhi ya wadau wa Elimu akifuatilia kwa makini hotuba ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ya mapato na matumizi  kwa mwaka wa fedha 2012/2013 iliyokuwa ikisomwa leo mjini Dodoma waziri wa wizara hiyo Dk. Shukuru Kawambwa  (hayupo pichani).

No comments: