Tangazo

August 8, 2012

Mabondia King Class Mawe na Mussa Sunga waingia kambini

Mabondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' (kushoto), akioneshana ufundi wa kutupa masumbwi wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya Ilala jana. www.superdboxingcoach.blogspot.com
KAMBI YA NGUMI ya Ilala jijini Dar es salaam ipo katika mazoezi ya kuwaandaa mabondia wake wawili watakaopanda ulingoni siku ya Iddi pili katika viwanja viwili tofauti.

 Akizungumza na waandishi wa habari Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi anaesimamia Kambi ya Ilala Rajabu Mhamila 'Super D' aliwataja mabondia hao kuwa ni Ibrahimu Class 'King Class Mawe' na Mussa Sunga .

Mapambano yao yanatarajiwa kufanyika katika uwanja wa Bandari Tandika Dar es salaam ambapo Mussa Seif 'Boda Boda' atapanda ulingoni Siku ya Idd Pili na wakati huo huo bondia Class atapanda ulingoni  katika ukumbi wa Diamond Jubilee kuzipiga na bondia Sako Mwaisege 'Dunga'.

 Aliongeza kuwa mabondia hao wapo katika mazoezi mazito wakisimamiwa na yeye mwenyewe na kocha mkongwe wa mchezo huo, Habibu Kinyogoli 'Master' pamoja na Kondo Nassoro.

Katika michezo hiyo kutakuwa na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo, Rajabu Mhamila 'Super D Boxing Coach' kwa ajili ya kuwapa mabondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

No comments: