Tangazo

August 8, 2012

MAKAMU WA RAIS DK. BILAL AFUNGA MAONYESHO YA SIKU YA WAKULIMA - NANE NANE MJINI DODOMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi kikombe Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Fatuma Salum Ally, baada ya Halmashauri ya Wilaya hiyo kuwa kuwa mshindi wa jumla katika maonyesho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane yaliyomalizika leo Agosti 8, 2012, wakati alipokuwa akifunga maonyesho hayo  katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma. Picha zote na Muhidin Sufiani-OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi mmoja kati ya wajasiliamali wa vikundi vya wakulima.

Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakhia Bilal, wakifurahia ngoma ya asili wakati walipowasili kwenye Viwanja vya Nzuguni. 

Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati alipomwakilisha Rais Jakaya Kikwete, kufunga rasmi maonyesho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane.

Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyesha Tuzo aliyokabidhiwa kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wa Rais katika kusimamia na kuendeleza Kilimo Kwanza.

No comments: