Tangazo

August 10, 2012

Uchaguzi Netiboli Dar wasogezwa mbele

Na Mwandishi Wetu

UCHAGUZI wa Chama cha Netiboli Mkoa wa Dar es Salaam (CHANEDA) uliokuwa ufanyike leo, sasa umeahirishwa hadi Agosti 17, mwaka huu.

Akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Michezo wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Adolf Halii, alisema kuwa kuahirishwa kwa uchaguzi huo kunatokana na ukumbi uliopangwa kufanyika tukio hilo kuwa na shughuli nyingine.

Alisema kuwa maandalizi yote ya uchaguzi huo, ikiwa ni pamoja na usaili, yalishakamilika, lakini ukumbi waliopanga kuutumia wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa, utatumika kwa shughuli nyingine ya ghafla hivyo kulazimiska kuuahirisha hadi siku hiyo.

"Imetulazimu kuahirisha uchaguzi huo wa netiboli Mkoa wa Dar es Salaam uliokuwa ufanyike kesho (leo) hadi Ijumaa ijayo baada ya ukumbi tuliopanga kuutumia kutumika kwa shughuli nyingine," alisema.

Aliwataka wajumbe wa mkutano huo wa uchaguzi pamoja na wagombea kuwa wavumilivu na kujiandaa kwa mchakato huo katika tarehe hiyo mpya iliyopangwa.

Halii aliwataja wagombea wanaowania nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo kuwa ni Winfrida Emmanuel (Mwenyekiti), Pili Mogella (Makamu Mwenyekiti), Joseph Ng’aza (Katibu Mkuu), Christina Mbetwa (Katibu Msaidizi), Anitha Lunogelo (Mhazini) na Michael Maurus (Ofisa Habari).

Wajumbe ni Zainab Mohamed, Mathew Kambona, Mussa Sambala, Khadija Ally na Georgina Kasembe.

No comments: