Tangazo

September 17, 2012

MAADHIMISHO YA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI YANAYODHAMINIWA NA AIRTEL TANZANA YANAANZA LEO

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, SACP  Mohamedi Mpinga (kushoto)  akipokea T-shirt kutoka kwa Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde zitakazotumika katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani inayofanyika kitaifa mkoani Iringa ambapo Airtel ni wadhani wakuu. Makabidhiano hayo yalifanyika katika ofisi za Makao Makuu ya Kikosi hicho jijini Dar es saalam. Kulia ni  Mrakibu Msaidizi  wa Polisi (ASP), Bonaventura Nsokolo.

Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde akizungumza na maafisa wa polisi mara baada ya makabidhiano.
*************************
·         Maadhimisho hayo kitaifa yanafanyika mkoani Iringa viwanja vya Samora

·         Airtel yakabidhi Fulana zenye Ujumbe maalum kwaajili ya kuhamasisha usalama barabarani


Kampuni ya simu za mikononi ya Airtel imeendeleza dhamira yake ya kushirikiiana na jeshi la polisi usalama barabarani katika kuhakikisha ajali za barabarani zinapungua na kudhibitiwa.

Wiki ya nenda kwa usalama barabarani inafunguliwa  kitaifa  mkoani Iringa katika viwanja vya Samora kuanzia tarehe 17-22 mwezi Septemba ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi  kwa niaba ya Mh, Raisi Jakaya Mrisho Kikwete.

akizungumza na wakati wa hafla maalum ya makabidhiano ya Fulana Ofisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde alisema "Airtel tunaona ni haki na ni sawa kuendelea kuthamini usalama barabarni na tunayo dhamira thabiti ya kuhakikisha tunaelimisha na kuhamasisha jamii na waendesha vyombo vya moto kuzingatia na kutii sheria za usalam barabarani, hivyo basi tunaomba watanzania kuunga mkono jitihada hizi ili kuhakikisha kwamba vyombo vya moto zinakaguliwa na kubandikwa stika maalumu za nenda kwa usalama barabarani".

Airtel inadhamini kampeni hii kwa miaka 4 mfululizo ambapo mwaka huu mbali na kuchapisha stickers imejitolea fulana 800 zenye thamani ya Tsh 8 zilizo na ujumbe maalumu kwa mwaka huu usemao“ Pambana na ajali za barabarani kwa vitendo, zingatia sheria”  makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi za makao makuu ya polisi usalama barabarini jijini Dar es saalam.

"Airtel Tanzania imeamua kuunga mkono kampeni hii ya nenda kwa usalama barabarani kwa sababu ya ongezeko kubwa la ajali za barabarani ambazo zinaathiri wateja wetu, aliongeza Bi. Matinde.

Bado Airtel haitaishia hapo tayari tumeshajipanga kufanya kampeni mbalimbali zitakazokuwa zikitoa elimu kwa watumiaji wa barabara hasa waenda kwa miguu na madereva wa vyombo vya moto kwa lengo la kupunguza ajali barabarani huku tukishirikiana na jeshi la polisi usalama barabarani.

Nae Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamedi Mpinga alisema "Ninawashukuru sana Airtel kwa ushirikiano wenu katika mkakati wetu wa kupunguza ajali barabarani, hadi sasa maandalizi yote ya wiki ya nenda kwa usalama yamekaa sawa na nawahamasisha sana wananchi wote wajitokeze katika vituo vyetu vyote nchini ili waweze kukagua magari yao na kujipatia stika za usalama barabarani.

Kwa mkoa wa Iringa ambapo ndiko tunafanya maadhimisho ya Usalama barabarani pia tutafanyia ukaguzi pale katika viwanja vya Samora vilevile  kituo cha polisi kati maeneo ya sokoni, kituo cha checkpoint Igumbilo na kile cha Mafinga,  alimaliza kwa kusema Kamanda Mpinga.

No comments: