Tangazo

September 12, 2012

Rais Kikwete katika ziara Rasmi ya Kiserikali ya siku tatu nchini Kenya

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete  akitembelea na kujionea shughuli mbalimbali za Taasisi ya Utatifi wa Kilimo ya Kenya (KARI). 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Mwai E. Kibaki wa Kenya pamoja na ujumbe wake wakiingia Ikulu ya Nairobi  Jumanne, 11 Septemba , 2012,  alipoanza Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu nchini humo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Mwai E. Kibaki wa Kenya wakipata picha ya kumbukumbu  Ikulu ya Nairobi  Jumanne, 11 Septemba , 2012,  alipoanza Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu nchini humo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Mwai E. Kibaki wa Kenya wakipata picha ya kumbukumbu  Ikulu ya Nairobi  Jumanne, 11 Septemba , 2012,  alipoanza Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu nchini humo. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania, Mhe Bernard Membe na kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Profesa Sam K. Ongeri.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete  pamoja na ujumbe wake na wenyeji wao wakianza  Mazungumzo Rasmi ya Kiserikali kati ya nchi hizo mbili.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi Jengo la Shule ya Ukarimu na Utalii ya Chuo Kikuu cha Kenyatta. Kulia kwake ni Waziri wa Elimu ya Juu, Mheshimiwa Margaret Kamar  na kuhsoto kwake ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Olive Mugendi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na wanafunzi baada ya  kufungua rasmi Jengo la Shule ya Ukarimu na Utalii ya Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akipozi na wanafunzi wawili waliotoa burudani ya vichekesho wakati wa sherehe za ufunguzi rasmi wa Jengo la Shule ya Ukarimu na Utalii ya Chuo Kikuu cha Kenyatta.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhiwa zawadi ya picha ya kuchora baada ya  kufungua rasmi Jengo la Shule ya Ukarimu na Utalii ya Chuo Kikuu cha Kenyatta. 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa na  Rais Mwai E. Kibaki, Waziri Mkuu wa Kenya Mhe Raila Odinga (kushoto) na Makamu wa Rais  wa Kenya Mhe Kalonzo Musyoka kabla ya  Dhifa ya Kitaifa  waliyoandaliwa na mwenyeji wao.

No comments: