Tangazo

September 18, 2012

Wahandisi kutoka Nchi 18 za Afrika watembelea McDonald Live Line Training Centre - Mvomero

Mkufunzi wa Live Line wa Kampuni ya McDonald Live Line Technology Ltd Donald Mwakamele (kulia), akitoa maelezo kuhusu vifaa mbalimbali vinavyohusu umeme kwa baadhi ya wahandisi 18 kutoka nchi mbalimbali za Afrika waliofanya ziara ya mafunzo katika Kituo cha Mafunzo cha McDonald Live Line kilichopo Dakawa Wilayani Mvomero Mkoa wa Morogoro hivi karibuni ili kujionea  kwa vitendo jinsi teknolojia ya ukarabati wa miundombinu ya umeme bila ya kukata nishati hiyo, ijulikanayo kama 'Liveline', inavyofanya kazi.

Wahandisi hao ambao walikuwa wakihudhuria mkutano mkubwa wa Sekta ya Umeme Afrika Mashariki (EAPIC), uliofanyika jijini Dar es Salaam Septemba 10-13, na kuwakutanisha watendaji wakuu wa makampuni 26 kutoka nchi mbalimbali zinazojihusisha na nishati ya umeme katika bara la Afrika.

CHINI: Ni mtiririko wa matukio mbalimbali ya ziara ya mafunzo ya wahandisi hao. PICHA ZOTE/DAILY MITIKASI BLOG






Kikosi kazi cha Wanahabari walioambatana na Wahandisi hao Mkoani Morogoro: (Kutoka kulia) ni John Badi (IPP Media & Daily Mitikasi Blog), Harriet Makweta (Mwananchi), Job (Jambo Leo), Khadija Kalili (Tanzania Daima & Bongo Weekend Blog), Jerome Risasi (Clouds TV & Radio), Kambi (Mtanzania), Peter Shadrack (Channel Ten) na Bashir Nkoromo (Uhuru & Daily Nkoromo Blog), katika picha ya pamoja nje ya Hoteli ya Nashera mkoani Morogoro muda mfupi kabla ya kuanza safari ya Mvomero.

1 comment:

ray njau said...

Hongera sana kwako muasisi na mtendaji mkuu wa asasi hii muhimu sana katika hizi zama za sayansi na teknolojia.Ni wajibu wa mamlaka husika kumuunga mkono ili uwekezaji katika asasi hii uongezeke kwa manufaa ya jamii yetu.