Mkurugenzi
Mtendaji wa Baraza la Biashara la Jumuia ya Afrika Mashariki, Andrew Luzze
Kaggwa, akizungumza wakati wa mafunzo ya siku tatu ya waandishi wa habari juu
ya Wajibu wa Vyombo vya Habari katika kuangalia Utekelezaji wa Masuala ya Soko
la Pamoja. Mafunzo hayo yanahusisha wanaandishi wa habari kutoka nchi zote
wanachama wa EAC, na kufanyika Ubungo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Baraza la Biashara la Jumuia ya Afrika Mashariki, Andrew Luzze
Kaggwa, akizungumza wakati wa mafunzo ya siku tatu ya waandishi wa habari juu
ya Wajibu wa Vyombo vya Habari katika kuangalia Utekelezaji wa Masuala ya Soko
la Pamoja. Wengine pichani ni washiriki wa mafunzo hayo.
Katibu wa baraza
la Asasi za Kijamii la Jumuia ya Afrika Mashariki, Dk. Martin Mwodha,
akizungumza katika mafunzo hayo juu ya ushiri wa Asasi za kiraia katika
ulelimishaji na ufikishaji wa elimu ya Soko la Pamoja la EAC.
Mchambuzi wa
Siasa za Afrika ambaye pia ni Mwanahabari Mkongwe nchini Tanzania, Jenerali
Ulimwengu akitoa mada katika mafunzo hayo leo.
Dawati
la ufundi nalo wakati wote lilikuwa katika wakati mgumu wakuhakikisha
kila kitu kinaenda sawa. Kutoka kushotoni Aline Ellermann, Elizabeth
Wanyoike na Hussein Karim wote kutoka ofisi ya GIZ ambao ndio
wawezeshaji mafunzo hayo yaliyoandaliwa pamoja na AC
Kuna
wakati mambo yanaonekana hayaendi na hapa anaonekana Elizabeth Wanyoike
(kulia) akikuna kichwa) huku Aline Ellermann akiendelea na kazi.
Fiona
Mbabazi kutoka Rwanda akimshukuru Ofisa mtendaji wa EABC, Andrew Kaggwa
kwa maelezo juu ya Baraza hilo.Kati ni Jenerali Ulimwengu na Aline
Ellermann.
Bizimana
Jean-Marie akitoa zawadi kwa Dk. Martin Mwadha wa Asasi za Kiraia za
EAC, wengine pichani kutoka kushoto ni Elizabeth Wanyoike wa GIZ,
Balozi Jeremy Ndayiziga, Andrew Kaagwa na Jenerali Ulimwengu.:Picha zote na Mroki Mroki wa Father Kidevu Blog
No comments:
Post a Comment