Dar es Salaam.
Mahakama ya Rufani Tanzania, imethibitisha Aeshi Hilaly kuwa mbunge halali wa Sumbawanga Mjini baada ya kushinda rufaa aliyokata kupinga hukumu ya Mahakama Kuu, Kanda ya Sumbawanga, iliyomvua ubunge.
Hilaly alivuliwa ubunge na aliyekuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, Bethuel Mmila Aprili 30, 2012, kutokana na kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa kiti hicho katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2010 kupitia Chadema, Nobert Yamsebo. Hata hivyo, Aeshi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) walikata rufani kupinga hukumu hiyo na zote zilisikilizwa kwa pamoja na jopo la Majaji watatu, Edward Rutakangwa, Profesa Ibrahim Juma na Steven Bwana.
Hukumu hiyo iliandikwa na Profesa Juma na kusomwa na Naibu Msajili wa Mahakama Rufani, Zahra Maruma.
Awali, mahakama hiyo ilitupilia mbali pingamizi lililowekwa na mjibu rufaa akidai kuwa warufani hawakuwa wamelipa gharama za kufungua taarifa ya kusudio la kukata rufaa, gharama za kumbukumbu za rufani na ada ya kukata rufaa.
Katika pingamizi hilo, pia mjibu rufaa alikuwa akihoji uhalali wa warufani kukata rufaa baada ya rufaa yao awali kutupiliwa mbali na kwamba taarifa ya kusudio la kukata rufaa waliyompa ilikuwa ni tofauti na waliyoiambatanisha kwenye rufaa.
Hata hivyo, Mahakama ilitupilia mbali hoja zote hizo za pingamizi ikisema licha ya kwamba hazina msingi wa kisheria, lakini pia kumbukumbu za rufaa zinaonyesha kuwa mambo hayo yaliyolalamikiwa yametekelezwa.
Hoja za rufani
Baada ya kutupilia mbali pingamizi hilo, Mahakama iliingia katika hoja za rufani na mbili kati ya tatu zilitosha kumrejesha Hilaly bungeni.

Hoja hizo ni madai ya mjibu rufaa, Yamsebo kufanyiwa vurugu katika mikutano yake ya kampeni kwenye vijiji viwili, na tuhuma za Hilaly kujihusisha na vitendo vya rushwa.
Katika uamuzi wake, Mahakama ilikubaliana na hoja za mawakili wa warufani na kusema kwamba baada ya kutathmini upya ushahidi katika kesi ya msingi, imebaini kuwa mlalamikaji hakuweza kuthibitisha madai yake kwa kiwango kinachohitajika kisheria bila kuacha shaka yoyote.
Mahakama ya Rufani ilisema imebaini kulikuwa na mkanganyiko mkubwa katika ushahidi wa mlalamikaji pamoja na mashahidi wake na kwamba Mahakama Kuu ilikosea kusema kuwa mkanganyiko huo haukuwa na athari na kwamba mlalamikaji amethibitisha madai yake.
“Tumebaini kuwa mjibu rufani, alishindwa kuthibitisha madai yake bila kuacha shaka na tunasema kuwa mjibu rufaa wa nne (Hilaly) alichaguliwa kihalali kuwa Mbunge wa Sumbawanga Mjini.
Baada ya kuridhika na hoja hizo mbili za vurugu kwenye kampeni na rushwa kuwa mlalamikaji alishindwa kuthibitisha na ambazo ndizo hukumu ya Mahakama Kuu ilizosimamia, Mahakama ya Rufani ilisema haina haja ya kuendelea na hoja ya tatu ya rufani.
Hoja hiyo ni kwamba mjibu rufani (Yamsebo) katika kesi ya msingi hakulipa dhamana ya kufungua kesi kama inavyotakiwa na Sheria ya Uchaguzi ya Mwaka 2010.
Baada ya hukumu
Hukumu hiyo iliamsha shangwe kwa wafuasi wachache wa Hilaly waliokuwapo mahakamani hapo ambao walimbeba juujuu huku wakiimba... “Tumeshinda, tumeshinda, CCM oye, CCM oye.”
Wafuasi wa Chadema walitoka mahakamani kimyakimya na Yamsebo alipotoka nje ya lango kuu la mahakama hiyo alisimama pembeni mwa Barabara ya Kivukoni na kuwapigia simu watu ambao hata hivyo hawakufahamika mara moja akiwajulisha kilichotokea na kuwataka wasambaze habari hizo kwa wengine... “Amerudishiwa ubunge wake, sambazeni hizo taarifa.”
Akizungumzia hukumu hiyo Hilaly alisema mahakama hiyo imetenda haki na kuwataka wananchi wa jimbo lake watulie... “Kila jambo lina mwanzo na mwisho wake. Nilipokuwa nje mambo mengi yalikuwa yamesimama, lakini sasa nimerejea jimboni kwangu kuwatumikia wananchi.”
Kwa upande wake Yamsebo alisema hukumu hiyo imemuumiza kwani hakuitegemea... “Nimesikitika, kwani mambo yote tuliyozungumza (tuliyokuwa tukilalamikia) yalitokea lakini sheria imempa ushindi. Nasema asante kwa sababu kila linalotokea Mungu amependa.”
Mkosamali ashinda rufani
Mbunge wa Muhambwe (NCCR- Mageuzi), Felix Mkosamali ameshinda rufani yake baada ya Mahakama ya Rufani kutupa maombi yaliyowasilishwa dhidi yake na aliyekuwa mgombea wa CCM, Jamal Abdallah Tamim.
Akisoma uamuzi huo Jaji Themistocles Kaijage alisema Mahakama ya Rufani imekubaliana na mlalamikiwa kuwa mrufani hakutimiza masharti ya kisheria ikiwamo kukosekana kwa kumbukumbu muhimu katika hati asilia ya malalamiko.
Chanzo: Mwananchi Mei 07,2013
No comments:
Post a Comment