May 7, 2013

Airtel yatoa msaada wa Vitabu kwa Shule Nne za Sekondari mkoani Tanga

Meneja Mauzo wa Airtel mikoa ya Tanga na Kilimanjaro, Bw. Edmund Lasway (wa tatu kulia), akikabidhi baadhi ya vitabu vya sekondari kwa Afisa Elimu wa wilaya ya Korogwe, Shaaban Shemzighwa  ikiwa ni msaada ulitolewa na kampuni yake kwa ajili ya kuchangia elimu kwa shule nne za sekondari mkoani Tanga katika hafla iliyofanyika katika Sekondari ya Korogwe Girls hivi karibuni. Shule zitakazonufaika na msaada huo ni Korogwe Girls, Mkuzi Juu, Kwendimu na Magila. Kulia ni Mkuu wa Shule ya Korogwe Girls, Bi Anesia Mauka.

Afisa Elimu wa wilaya ya Korogwe, Shaaban Shemzighwa ikikabidhi sehemu ya vitabu vilivyotolewa kwa lengo la kuchangia elimu toka kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kwa Mkuu wa shule Korogwe Girls, Bi Anesia Mauka.
*********
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imetoa msaada wa  itabu vya Hesabu, Kemia na baolojia vyenye thamani ya shilingi milioni 12, kwa shule nne za mkoa wa Tanga. 

Msaada huo ni sehemu ya mpango wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel  wa kusaidia ukuaji wa sekta ya limu kupitia kampeni yake ya shule yetu.

Akipokea vitabu hvyo kwa niaba ya shule za mkoa wa tanga afisa elimu wa wilaya ya korogwe Bw. Shaaban Shemzighwa alisema,“ tunawashukuru Airtel kwa msaada huu wa vitabu kwani utasaidia kupunguza tatizo lauhaba wa  vitabu kwa shule zilizopatiwa msaada huo na kuongeza kiasi cha ufaulu kwa wanafunzi. Tunaomba juhudi hizi zisihishie hapaziendelea katika shule mbalimbali mkoani hapa na mikoa mingine yaTanzania ili kuondoa ujinga na umaskini na kuwapa watoto wetu elimu bora kwani hawa ndio taifa la kesho.

Kwa upande wake meneja mauzo wa Airtel mikoa ya Tanga na  Kilimanjaro Bw. Edmund Lasway amesema msaada huo ni sehemu ya mpango wa kampuni yake wa kusaidia ukuaji wa elimu hapa nchini. Chini ya mpango maalumu wa Shule yetu tumeweza kuzifikia shule nyingi za sekondari nchini.

Akiongea kwa niaba za shule zilizopokea msaada huo Mwalimu mkuu wa shule ya secondari ya Mkuzi juu Bwn Victor Mwenda alisema”  Tunatoa shukurani kwa Airtel kwa msaada wa vitabu katika shule zetu zasekondari, kwa hatua hii itasaidia kupunguza tatizo la vitabu linalozikabili na kuongeza ufanisi katika masomo ya sayansi. Tunawaomba wanafunzi wavitunze na kuvitumia vizuri hivi vitabu kwani ni nyenzo muhimu katika elimu ya sekondari.

Vilevile Meneja wa huduma za jamii wa Airtel Tanzania Bi Hawa Bayuni alidokeza kuwa Airtel iko katika mkakati wa kuanza awamu nyingine ya ugawaji wa vitabu kwa shule za sekondari kwenye kila mkoa ikiwa ni program yake ya mwaka huu ya kurudisha kwa jamii kupitia elimu “tunaingia katika awamu ya mpya ya utowaji wa vitabu kwa shule ngingi zaidi  kila mkoa hapa Tanzania, mradi wetu huu utazingatia zaidi shule za sekondari zilizopendekezwa na Wizara ya Elimu kwamba ni shule zipi zina uhitaji  mkubwa wa vitabu na kushauri  ziingie katika mpango wa kusaidia jamii wa Airtel shule yetu” alieleza Bayumi.
 
Airtel toka tulivyooanza mradi huu wa Vitabu miaka nane iliyopita tumeweza kuzifikia zaidi ya shule 1500 za sekondari zilizopo Tanzania kwa kutoa msaada sawa kwa mikoa  yote  na kuwafikia wanafunzi katika kila kona ya Tanzania na pia kukarabati miundombinu ya shule kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini ikiwa ni hatua ya Airtel kukuza kiwango cha elimu kwenye maeneo mbalimbali Tanzania aliongeza Bayumi.

Shule zilizofaidika na msaada wa vitabu hivi mkoa ni Tanga ni pamoja na shule ya sekondari ya Korogwe Girls, Mkuzi Juu, Kwendimu na Magila.mkakati ni kuendelea kutoa vitabu kwa shule mbalimbali nchini ambapo droo ya shule za sekondari zitakazo faidika na vitabu kwa mwaka huu wa 2013 -2014 itafanyika mwenzi Juni  na kutoa nafasi kwa shule nyingine nyingi za sekondari nazo kufaidika na mpango huu wa Airtel shule yetu.

No comments:

Post a Comment