May 3, 2013

Hatimae Marehemu Adolf a.k.a Brian aka Thadeo Lwakajende apumzishwa katika nyumba ya milele





Picha mbalimbali za misa hadi mazishi ya Marehe Adolf.
Watanzania waishio New jersey na New York wanapenda kutoa shukrani zao za dhati kwa wale wote waliotoa ushirikiano mkubwa  katika kipindi chote kigumu cha msiba hadi mazishi ya Marehemu Adolf a.k.a Brian aka Thadeo Lwakajende.

Aidha wametoa shukrani za pekee kwa ajili ya blog za watanzania zilizoweza kufikisha habari za msiba wa marehemu Adolf aka Brian aka Thadeo Lwakajende kwa watu wengi sana kwa muda mfupi sana kuliko tulivyotegemea.

Kwa ushirikiano huo waliweza kufanikiwa na kuweza kukamilisha shughuli hiyo kwa kipindi kifupi sana kuliko walivyokua wakitarajia.

Adolf alipelekwa kulazwa katika nyumba yake ya milele Jumatano Mei 01, 2013 huko katika makaburi ya Mt Pleasant, Hawthorne, NY 10532

Asanteni sana

Imetolewa na Pauline



No comments:

Post a Comment