Tangazo

May 6, 2013

Majina ya Wanamichezo watakaoshiriki Tuzo za Wanamichezo Bora wa Taswa 2012 yatajwa

Haji Manara
KAMATI ya kusimamia Tuzo za Wanamichezo Bora wa Tanzania mwaka 2012 zinazotolewa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) imepokea mapendekezo ya majina ya wanamichezo kutoka vyama mbalimbali kwa ajili ya kuwania tuzo hizo kwa kila mchezo.

Majina ya wanamichezo hao yamependekezwa na vyama husika, isipokuwa mpira wa miguu kwa wanaume pamoja na mpira wa kikapu, ambapo majina yameteuliwa na kamati kwa kushirikiana na baadhi ya wahariri wa habari za michezo na wadau wa michezo husika, ingawa awali vyama hivyo viliombwa kuwasilisha majina lakini havikutekeleza ombi hilo hivyo kamati ikaamua kutafuta utaratibu mwingine wa kupata majina.

Pia vyama viwili vya michezo ya  paralimpiki na baiskeli bado majina hayajaifikia kamati yetu kutokana na sababu mbalimbali na tayari wameahidi watawasilisha majina hayo kabla ya Mei 12 mwaka huu. Chama cha Mpira wa Wavu pia kimeshindwa kuwasilisha majina.

Hatua ya mwisho ambayo itafanyika baada ya kupokea mapendekezo hayo kwenye kila mchezo, Kamati ya Tuzo za Taswa itafanya uchambuzi kupitisha majina hayo kulingana na sifa ambazo vyama husika vimeleta kwa kila mwanamichezo na kuona kama wanastahili kupewa tuzo kulingana na vigezo vya kamati na TASWA.

Awali TASWA ilipanga tuzo hizo zifanyike Aprili 27 mwaka huu, lakini imeshindikana kutokana na sababu mbalimbali zilizokuwa nje ya uwezo wa Kamati ya Tuzo pamoja na chama kwa ujumla na sasa sherehe zitafanyika mwanzoni mwa mwezi Juni katika tarehe itakayotangazwa baada ya kukubaliana na wadhamini, ambapo mazungumzo yanatarajiwa kukamilika kabla ya Mei 15 mwaka huu.

Tunavishukuru vyama vyote vilivyotupa ushirikiano kwa hatua ya awali kwa kutupatia mapendekezo yao pamoja na kutaja sifa kwa kila mchezaji waliyewasilisha jina lake nasi tunaahidi tutapitia kwa umakini mapendekezo hayo, lakini uamuzi wa kamati ndiyo utakaokuwa wa mwisho.

TASWA itatoa tuzo kwa kila mchezo ambao kamati yetu ambayo  Katibu wake ndiye pia Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando itajiridhisha wanastahili, ambapo baadaye washindi wa kila mchezo watawania Tuzo ya Mwanamichezo Bora wa Tanzania kwa Mwaka 2012.Tuzo ya Mwanamichezo Bora wa Tanzania kwa mwaka 2011 ilienda kwa Shomari Kapombe. Washindi wengine kwa miaka ya karibuni ni Mwanaidi Hassan (2010 na 2009), Mary Naali (2008), Martin Sulle (2007) na Samson Ramadhan (2006).

Majina ya wanaowania kwa mwaka 2012:

 MPIRA WA MAGONGO-WANAUME

1 Sylvester Kigodi

2.   Casto Mayuma

3.   Gurtej Bilu Singh

4.   Vendri Bhamra

5. Elias Samala


GOFU YA KULIPWA

1 Hassani Kadio

   2 Yassin Salehe

  3 Fadhili Nkya

  4 Salimu Mwanyenza

  5 Rajabu Iddy

 GOFU YA RIDHAA WANAWAKE:

 1:MADINA IDDI

2:ANGEL EATON

3. HAWA WANYECHE

4.AYNE MAGOMBE

 GOFU YA RIDHAA WANAUME

Jimmy Mollel

Frank Roman

Nuru Mollel

Martin MacDonald

John Said

 NGUMI ZA RIDHAA-WANAUME

    Ismail Isack Galiatano
    Said Hofu
    Selemani Kidunda.
    Victor Njaiti
    Mohamed Chibumbui.

 NGUMI ZA RIDHAA WANAWAKE:-

1.   Sara Andrew

2.   Irene Kimaro

3.   Easter Kimbe.

4.   Mather George

5.   Mariam Nyerere.

 NGUMI ZA KULIPWA

1.      Francis Miyeyusho

2.     Ramadhan Shauri

3.     Thomas Mashali

4.     Said Mbelwa

5.     Francis Cheka

JUDO-TANZANIA BARA-WANAUME

1)     AHMED MAGOGO

2)    ADREW THOMAS MLUGU

3)    GEOPHREY EDWARD MTAWA

4)    GERVAS LEONARD CHILIPWELI

5)    ABUU SELEMANI MCHETEKO

6)   ABUUBAKAR NZIGE


JUDO TANZANIA BARA WANAWAKE

1.     MATRIDA .H. TEMBA

2.     AMINA MOHAMED


JUDO ZANZIBAR-WANAUME

1.    MOHAMMED KHAMIS JUMA

2.   MASOUD AMOUR KOMBO

3.   MBAROUK SULEIMANI SULEIMAN


JUDO ZANZIBAR-WANAWAKE

1.     GRACE ALPHONCE

2.     LAYLATI MOHAMMED

 TENISI-WANAWAKE

 [1] Rehema Athumani

[2] Vailety Petar

 [3] Mkunde iddi

 [4] Edna John

 [5] Zuhura Baraka

TENISI  Wanaume

 [1] Omary Abdalah

 [2] Yassini Shabani

 [3] Hassan Kasimu

 [4] Kiango Kipingu

 [5] Lebric Jacobu

 MPIRA WA MIKONO-WANAUME

Faraji Shaibu
Nyuki ZANZIBAR

Hemedi Salehe
JKT

Abinery  Kusena
JKT

Ally Khamis
Ngome

Hassani  Yusufu
Magereza

MPIRA WA MIKONO-WANAWAKE

Catherine    Mapua
Ngome

Dorisi        Mangara
Magereza

Zakia        Mohamed
Ngome

Happy      Mahinya
JKT

Mary       Kimiti
Magereza


RIADHA-WANAWAKE

1.Zakia Mrisho

2. Mary Naali

 3.Jacklin Sakilu

4.Sarah Ramadhani 
 5.Anjelin Tsere

6. Sara Maja


RIADHA-WANAUME

1. Dickson Marwa

 2. Faustine Musa

3. Augstino Sule

4. Bazil John

5. Samson Ramadhan

KRIKETI-WANAUME

1.   Abhik Patwa.

2.     Benson Mwita.

3.     Sefu Khalifa.

4.     Issa Kikasi.

5.   Riziki Kiseto

KRIKETI-WANAWAKE

Monica Pascal.

Mwanaiddi Ibrahim.

Hadija Nasibu

Esther Wales

Mwanaidi Ammy



SOKA-WANAWAKE

FATUMA MUSTAPHA

ASHA RASHID

MWANAHAMISI OMARY

SOPHIA MWASIKILI

ESTER CHABRUMA



SOKA-WANAUME

JOHN BOCCO-AZAM

KELVIN YONDANI-YANGA

SHOMARI KAPOMBE-SIMBA

MCHA KHAMISI-AZAM

MBWANA SAMATTA-TP MAZEMBE

Thomas Ulimwengu-TP Mazembe



WACHEZAJI WA NJE WANAOCHEZA TANZANIA

EMMANUEL OKWI-SIMBA(SASA ETOILE DU SAHEL)-SOKA

KIPRE TCHETCHE-AZAM-SOKA

HARUNA NIYONZIMA-YANGA-SOKA

HAMISI KIIZA-YANGA-SOKA

MARY WAYA-FILBERT BAYI –NETIBOLI (ALIKUWA KOCHA MCHEZAJI)



KIKAPU-WANAWAKE

Faraja Malaki- Jeshi

Evodia Kazinja-JKT Stars

 Sajida Ahmed-Don Bosco

Rehema Kilomba-Donbosco

Tukusubira David-Vijana Queens

 KIKAPU-WANAUME

Mussa Chacha-Savio

Lusajo Samuel Mwakipunda-Oilers

Salim Mchemba-ABC

Filbert Mwaipungu-ABC

Steven Atanasio-ABC



NETIBOLI

Lilian Sylidion-Filbert Bayi

Mwanaidi Hassan-JKT

Irene Elias Kanile-Filbert Bayi

Jacqueline Sikozi-Filbert Bayi

Faraja Malaki-Jeshi Stars



WACHEZAJI BORA CHIPUKIZI



Salum Abubakari-Azam-soka

Frank Domayo-Yanga-soka

Edward Cristopher-Simba-soka

Emmanuel Malya-Tenisi Gymkhana Arusha

Tambwe Juma-Kriketi


WATANZANIA WANAOCHEZA NJE

Mbwana Samatta-TP Mazembe

Ivo Mapunda-Gor Mahia

Hasheem Thabeet-Oklahoma

Thomas Ulimwengu-TP Mazembe

Soud Abdulrazak-Uganda (kikapu)

Mohammed Abdallah ‘dulah’-Uganda (kikapu)

 TUZO YA HESHIMA--- ITATANGAZWA UKUMBINI

TUZO YA MWANAMICHEZO BORA MWAKA 2012- ATAPATIKANA MIONGONI MWA WASHINDI WA KILA MCHEZO
 
Imetolewa na
Haji Manara
Mwenyekiti Kamati ya Tuzo TASWA

No comments: