MWENYEKITI wa Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi
Taifa (UVCCM), Sadifa Juma Hamisi, amepinga vikali kuwepo kwa mfumo wa serikali
tatu kama inavyopendeka rasimu ya katiba.
Sadifa ameyasema hayo wakati akizungumza na
wanachama wasomi wa UVCCM kutoka katika vyuo vikuu mkoani kilimanjaro katika
hafla ya kuwaaga wasomi hao na ambapo pia ametunuku vyeti vya uanachama kwa wanafunzi
312 pamoja na kuwakabidhi kadi za uanachama wanachama wapya.
Mwenyekiti
wa UVCCM Kilimanjaro akiongoza maandamano kuelekea katika ukumbi wa CCM
mkoa ambapo ndipo ilikofanyikia mkutano mkubwa wa UVCCM jana
|
Mwenyekiti huyo ambaye pia ni mbunge wa jimbo la
Donge (CCM) zanzibar, amesema uwepo mfumo wa serikali tatu ni mzigo mkubwa
kwani kutokana na uduni wa uchumi wan chi yetu itakuwa vigumu kuendesha serikali
tatu kwa maana ya serikali ya Zanzibar, serikali ya Tanzania bara na ule wa
muungano.
Viongozi waandamizi wa CCM mkoani Kilimanajro katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa
|
“Jamani tusidanganyane, kuendesha serikali tatu ni
mzigo, kwa uduni wa uchumi wetu sidhani kama itakuwa rahisi kuendesha serikali
tatu, kama kutakuwa na serikali tatu kuna hatari ya kuvunjika kwa muungano wetu
huu maana uwezo kuchangia hatuna, tutajiingiza kwenye matatizo makubwa, vijana
tuwe makini na tutumie taaluma zetu kuhimiza umuhimu wa kuwepo kwa muungano huu
wa sasa,"
Mwenyekiti
wa UVCCM Taifa, Sadifa Juma Hamisi Akipokea Maandamano ya Wanafunzi wa
Vyuo vikuu Kilimanjaro ambao ni makada wa UVCCM mkoani Kilimanjaro
|
Aidha Sadifa amewahimiza vijana kuwa mfano mzuri kwa
jamii huku akiwahimiza kuwa waadilifu, wazalendo, kujiamini na kuwa na nidhamu
hali ambayo itasaidia kuwepo kwa amani na usalama wa nchi.
Amesema bila amani na muungano wa wananchi maendeleo
hayawezi kupatikana katika nchi ambpo aliwataka vijana kuwa mtari wa mbele
kuwaelimisha wananchi wa kawaida juu ya umuhimu wa kuenzi, kudumisha na kuimarisha
muungano wa zanzibar na Tanganyika kama
njia pekee ya kuhakikisha nchi inakuwa na amani siku zote.
Katibu wa UVCCM manispaa ya Moshi, Bwana Makwaiya akisakata Rumba muda mfupi baada ya maandamano kuwasili katika makao makuu ya CCM mkoa wa kilimanjaro
|
“Vijana tuna wajibu kubwa wa kuwaenzi waliotuletea
muungano wetu wa sasa, taaluma zetu ziwe dira ya jamii katika kuenzi, kudumisha
na kuimarisha muungano wetu kwani ndio njia pekee ya kusaidia kudumisha amani
na usalama wan chi yetu, tuepuke kujiingiza katika mkumbo wa wale wanaodai nchi
haitatawalika,” amesema
Hata hivyo Sadifa amewataka vijana kutodanganyika na
vyama vinavyoeneza chuki na maandamano yasiyokuwa na msingi wowote huku
akifafanua kuwa kisheria kuandamana na haki ya msingi lakini ifuate sheria na
yassingilie haki za wengine.
Sadifa
akikabidhi cheti cha unachama kwa mwanafunzi wa chuo kikuu muccobs
jana, jumla ya wanavyuo 312 walipata vyeti vya uanachama wa UVCCM
|
“Chama pekee katika nchi hii ni CCM, kuna vyama
vingine vimeanzishwa ambavyo mimi binafsi naviita ‘Saccos’, hauwezi
ukajikopesha fedha kienyejienyeji kama alivyofanya Dk. Slaa! Vijana tuwe makini
na saccos hizi ambazo ajenda zao ni kukopeshana na vurugu tu,” amesema Sadifa
Kwa upande wake mwenyekiti wa shirikisho la wanafunzi
wa vyuo vikuu wanachama wa CCM kilimanjaro, Wakati Mtulya akizungumzia
changamoto wanazokumbana nazo, alisema kumekuwa na urasimu ndani ya bodi ya
mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, ambapo mikopo imekuwa ikitolewa kwa watu
wasiostahili huku walengwa wakiendelea kutaabika.
Amesema kuwa kumekuwa na mchezo ndani ya bodi hiyo,
ambapo mikopo imekuwa ikitolewa kwa watoto wa matajiri huku wastahili ‘watoto
wa wakulima’ wakibaki kuzungushwa na kuwekewa masharti magumu ya kupata mikopo
hiyo jambo ambalo limekuwa likichangia kuwepo kwa vitendo vibaya miongoni mwa
wanafunzi hao.
Sadifa (aliyevaa suti) akiongoza vijana kucheza kwaito katika ukumbi wa CCM mkoa wa Kilimanjaro
|
“Mikopo ni yetu, sio ruzuku, lazima tukopeshwe kwa
wakati kwani lazima tutairudisha lakini jambo la kusikitisha, bodi hii imekuwa ikitoa
mikopo kwa watoto wa masaki, huku sisi watoto wea mkulima tukiendelea
kuzungushwa na kuwekewa masharti magumu ili kupata mikopo hiyo, hili ni tatizo,”
amesema Mtulya (habari na TAIFA LETU.com).
No comments:
Post a Comment