Tangazo

August 22, 2013

Mkutano wa Kitaifa wa Baraza la Katiba la Tasnia ya Habari

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba akizungumza wakati wa Mkutano wa Kitaifa wa Wajumbe wa Baraza la Katiba la Tasnia ya Habari lililoundwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT), uliofanyika jijini Dar es Salaam Agosti 20.2013. Wajumbe wa baraza hilo kutoka kanda sita nchini walikutana kufanya majumuisho ya mapendekezo ya jinsi ya kuboresha Rasimu ya Katiba ya Mpya ya Tanzania wakijikita zaidi katika masuala ya Haki ya Kupata Habari, Uhuru wa Vyombo vya Habari na Haki ya Kujieleza. Kushoto ni Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga na Meneja Udhibiti na Viwango wa MCT, Bi. Pili Mtambalike. PICHA ZOTE/JOHN BADI

Sehemu ya Wajumbe wa Baraza hilo wakiwa katika mkutano.

Wajumbe wa baraza hilo (kutoka kushoto), Apolinary Tairo (The Express), Felix Kaiza (Kituo cha Habari za Uwekezaji wa Utalii Tanzania) na Fili Karashani (Tanzania Press Center).
Mjumbe wa Baraza hilo anayewakilisha Morogoro Press Club na Mtangazaji wa ITV/Radio One, Idda Mushi akichangia hoja.

Naibu Katibu Mkuu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba,Casmir Kiuki akifafanunua jambo wakati wa mkutano huo.
Jaji Warioba akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza hilo.

No comments: