![]() |
Na Magreth Kinabo
Rais Jakaya Kikwete amesema kwamba Tanzania haina mpango wa kujitoa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)
na itaendelea kuwepo kwa kuzingatia
matakwa ya mkataba wa EAC na Itifaki zake,licha ya kutoshirikishwa kwa baadhi
ya mambo.
Aidha Rais Kikwete
amesisitiza kuwa Tanzania ni kati ya zile nchi zinazotaka ngazi zote za mchakato wa
utengamano zitekelezwe moja baada ya nyingine bila kuruka hata moja na kuongeza
kuwa huo sio msimamo wake au Serikali pekee
bali ndio Watanzania walio wengi.
Kauli hiyo ilitolewa leo Bungeni mjini Dodoma wakati Rais Kikwete
alipolihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu msimamo wa
Tanzania juu ya EAC.
“Napenda kuwahakikishia
waheshimiwa wabunge kuwa hatuna
mpango wa kutoka (kama vijana wasemavyo hatoki mtu hapa). Tupo na tutaendelea kuwepo!,” Napenda kuwahakikishia
kuwa Tanzania itaendelea kushiriki katika shughuli za EAC na kuimarisha
utengamano wa Afrika Mashariki .
“Tutafanya kila tuwezalo kuhakikisha kuwa jumuiya
haidhoofiki wala kufa. Na iwapo
itadhoofika au kufa kamwe hatutaki Tanzania inyooshewe kidole kuwa chanzo wala
kichocheo chake. Ndiyo maana,
hatutachoka kuzungumza na wenzetu kuhakikisha kuwa EAC inaendelea kustawi,” alisema Rais Kikwete.
Alisema kamati hiyo iliongozwa na Profesa Samwel Wangwe na
katika taarifa yake, ilieleza kuwa
asilimia 74.4 ya Watanzania wanaunga
mkono kuwepo kwa Shirikisho lakini ni asilimia 25.4 tu ndiyo waliunga mkono
kuharakishwa kwake.
Rais Kikwete
alisema ni lazima ni kutambua ukweli
kuwa kunufaika kiuchumi ndicho kichocheo kikubwa cha nchi kujiunga na kuendelea
kuwa mwanachama wa EAC.
Alisema Tanzania
itaendelea kukumbusha umuhimu wa kufanya mambo yanayojenga na kuepuka yale
yanayoweza kubomoa, kama vile kuheshimu matakwa na masharti ya mkataba
ulioanzisha EAC, Itifaki zake na maamuzi halali ya vikao rasmi na asasi za
jumuiya hiyo .
“Tukifanya hivyo Jumuiya ya Afrika ya Mashariki itadumu,
itazidi kustawi na kunufaisha nchi wanachama na watu wake kama yalivyo malengo
na madhumuni ya kuundwa kwake,” alisisitiza.
Rais Kikwete.
Alisema
msimamo na mtazamo wa nchi , kuundwa kwa Shirikisho iwe ndiyo hatua ya mwisho.
Akizungumzia kuhusu
kumekuwepo na madai Tanzania inachelewesha maendeleo ya jumuiya hiyo
alisema hayana ukweli wo wote.
Huku akiongeza
Tanzania haina tatizo na kuharakisha mchakato wa utengamano, lakini
inapata taabu kuruka baadhi ya hatua kabla hazijakamilika. Hivyo
alizitaka nchi uanachama kuwa
makini katika kila hatua tunayochukua.
Alisema kwa msimamo na mtazamo wa nchi ,
suala la Shirikisho liwe
ndiyo hatua ya mwisho.
Hata hivyo Rais
Kikwete alisema pengine msimamo wetu
kuhusu kuharakisha Shirikisho na masuala ya ardhi, ajira, uhamiaji,ndiyo
yanayotuletea vikwazo.
Hivi karibu viongozi wa nchi tatu wanachama wa EAC yaani Uganda, Rwanda na Kenya walikutana bila
ya ushiriki wa viongozi wa Tanzania na Burundi.
Viongozi wenzangu hao wamefanya mikutano mitatu yaani Juni 24-25 , 2013 mjini Entebbe, Uganda; Agosti 28, 2013 mjini Mombasa, Kenya na Oktoba 28 ,
2013 mjini Kigali, Rwanda.
No comments:
Post a Comment