Mgeni rasmi katika
hafla hiyo ya kukabidhi tuzo ya Daudi
Mwangosi Bw Tido Mhando wa tatu
kulia akimkabidhi mshindi mfano
wa hundi ya Tsh milioni 10
Absalom Kibanda tuzo yenye thamani ya Tsh milioni 10,0000 katikati ni mjane wa Mwangosi
Itika Mwangosi wa kwanza kushoto ni makamu wa rais wa UTPC Jane
Mihanji na rais wake
Keneth Simbaya.
*************************
Na Abdulaziz Video
Mwanza
Mhariri mtendaji wa Kampuni ya New Habari Absalom Kibanda jana amekabidhiwa tuzo ya Uandishi wa kishujaa na Utumishi
uliotukuka ya Marehemu Daud Mwangosi baada ya Mhariri huyo kukumbwa na
tukio la uvamizi na kisha kutobolewa jicho na watu wasiofahamika
Machi 6 mwaka huu.
Kabla ya
makabidhiano ya tuzo hiyo wadau wote wa habari wakasimama na kisha kuimba wimbo
maalumu wa kumuenzi Marehemu Daud Mwangosi.
Akizungumza na wadau wa habari Jijini Mwanza. Baada ya
makabidhiano hayo mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications
Tido Mhando amewahimiza waandishi wa habari kuendelea kupambana katika jitihada
za kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya Taifa. Kutokana na umuhimu wa tuzo
hii ya Marehemu Daud Mwangosi aliyeuwawa kwa kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu
la machozi lililolipuliwa visivyo September 2 mwaka jana kijijini nyololo
mkoani Iringa Mhando akatumia fursa hii kulaani vikali vitendo vya kuminya
uhuru wa habari vinavyofanywa na baadhi ya viongozi nchini.
Baada ya kibanda kukabidhiwa tuzo hiyo pamoja na hundi ya
shilingi millioni kumi akawapa moyo wa ujasiri waandishi wa habari
kote nchi wa kutonyamazishwa wakati wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao
licha ya kuwepo changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo zikiwemo za vitisho.
Kutokana na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya
habari nchini wadau wa habari wakiwemo wakongwe katika fani hii hawakubaki
nyuma kuelezea mitazamo yao kuhusu uelekeo wa sekta hii. Tuzo za uandishi wa
kishujaa na utumishi uliotukuka ya Marehemu Daud Mwangosi itakuwa ikitolewa
kila mwaka ili kutambua michango mbalimbali inayotolewa na waandishi wa habari
katika kutekeleza majukumu yao ya kikazi.
|
No comments:
Post a Comment