Meneja wa Huduma za Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kushoto),akikabidhi sehemu ya vitabu kwa Afisa Elimu vifaa na Takwimu wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Bwana Yalagwila Gwimo. |
Wanafunzi wa shule ya sekondari Gungu akifurahia
kupokea vitabu vya masomo ya sayansi kutoka kwa kamouni ya simu za mkononi ya
Airte.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
KIGOMA
Meneja huduma za Jamii wa Kampuni ya simu za
Mkononi ya Airtel Tanzania Bi Hawa Bayumi amesema nguvu kazi ya wananchi wenye
ujuzi na elimu inahitajika nchini, hivyo wanafunzi wa shule za sekondari wana wajibu
wa kuitumia elimu kama ngazi ya kuliwezesha taifa kuwa na maendeleo.
Bayumi aliyasema hayo wakati akikabidhi vitabu vya masomo ya Sayansi kwa Afisa Elimu vifaa na Takwimu wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Bwana Yalagwila Gwimo kwa ajili ya shule ya Sekondari ya Gungu Mkoani Kigoma, Bayumi amesema serikali haiwezi kufanya kila kitu,wanafunzi wanatakiwa kutumia fursa hii kupanua uelewa wao kupitia vitabu vinavyotolewa na kampuni yake.
“Sisi kama Airtel tumetekeleza jukumu letu la
kutoa vitabu kwa shule za Sekondari na tunatarajia wanafunzi mtasema kufeli
sasa basi baada ya kuwekewa mazingira mazuri ya kupata vitabu vya kiada na ziada”…Alisema
Bayumi.
Amesema taifa bado halijafikia kiwango cha
kujivunia cha kuwa na wasomi wengi wa fani ya Sayansi, hivyo Airtel inasisitiza
wanafunzi wafanye jitihada katika masomo hayo “Tunapotengeneza mazingira mazuri
kwa mwanafunzi pia tunatengeneza mazingira mazuri kwa waalimu kwa kutoa vitabu
vya kufundishia ambavyo vinakubalika na wizara ya elimu”Alisema Bayumi.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya
Sekondari Gungu Bwana Alberto Dobeye mbali na kuishukuru kampuni ya Airtel
chini ya mpango wa “Shule Yetu” kwa kutoa vitabu hivyo ameiomba serikali
kuharakisha ujenzi wa maabara shuleni hapo.
“Tunawashuru sana Airtel kwa vitabu hivi…lakini
mkubuke kupata vitabu ni jambo moja na maabara ni jambo jingine,serikali
ijitahidi kujenga maabara hapa shuleni ili wanafunzi wasome na kufanya
majaribio ya Vitendo” Alisema Mwalimu Dobeye.
Kwa upande wake Afisa Elimu vifaa na Takwimu wa
Manispa ya Kigoma Ujiji Bwana Yalagwila Gwimo amesema vizuri wanafunzi wakajikita
kusoma vitabu kwa lengo la kupanua ulewa wao na hivyo kuwa katika nafasi nzuri
ya kuongeza ufaulu.
Nao
Wanafunzi Kassim Abdallah, na Rosemary Christopher kwa kwa niaba ya
wenzao wameipongeza kampuni ya simu ya Airtel kwa msaada huo na kwamba vitabu hivyo
vitachochea Ari za wanafunzi kuongeza bidii katika masomo ili kufikia lengo la
ufaulu kwa kupata alama za juu.
Msaada huo wa Vitabu vilivyotolewa ni mwendelezo wa shughuli za huduma kwa jamii zinazotelewa na Airtel kupitia mradi maalumu wa Shule yetu unaoziwezesha shule mbalimbali kutapa vitabu vya kiada na kiada, mpaka sasa shule zaidi ya 1000 zimeshafaidika na mpango huo.
No comments:
Post a Comment