Tangazo

January 30, 2015

BARABARA KWENDA OLOLOSOKWAN TISHIO KWA MAGARI MAKUBWA

DSC_0035
Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues aliyemtembelea ofisini kwake wakati wa ziara ya kikazi ya siku nne kwenye kijiji cha Ololosokwani na halmashauri ya Ngorongoro kwa ajili ya maandalizi ya mradi wa kijiji cha digitali unaoendeshwa na Unesco kwa kushirikiana na Ki-elektronic ya Samsung unaotarajiwa kuwasili kijijini hapo mwezi februari ukitokea jijini Dar.

Na Mwandishi wetu, Ngorongoro

MKURUGENZI Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues ameonesha mashaka yake juu ya ubora wa barabara ambazo magari mazito yenye vifaa vya kijiji cha digitali Ololosokwan yanaweza kupita.
Alisema hayo kwenye mazungumzo na Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Elias Wawa Lali wakati alipomtembelea ofisini kwake.

Akiwa katika ofisi za mkuu huyo wa wilaya kumwelezea shughuli za Unesco katika wilaya yake, Mkurugenzi Mkazi huyo alipata nafasi ya kuzungumzia haja ya kuboreshwa kwa maaneo kadha ya barabara kuelekea kijiji cha Olosokwan ili kuyawezesha magari hayo makubwa kufika kwa urahisi.

Huku akimuonesha mkuu wa wilaya baadhi ya picha alizopiga akiwa njiani kukagua njia ya kupita magari hayo na kuangalia maandalizi ya mwisho ya mradi huo mkubwa na wa kipekee nchini alisema hali ya barabara si nzuri hata kidogo.

Vifaa kwa ajili ya kijiji hicho vipo bandarini tayari na magari yanayoweza kubeba makontena hayo ni makubwa na barabara za kuelekea kijiji hicho ni mbaya.
DSC_0041
Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali (katikati) akizungumza na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues (kulia) aliyeambatana na wataalamu wa elimu, afya na mawasiliano pamoja na Mratibu wa Taifa wa tiba asilia na mbadala katika Idara ya Tiba Wizara ya Afya na ustawi wa jamii. Dkt Liggy Vumilia (hayupo pichani) . Kutoka kushoto wa kwanza ni Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias, Afisa mipango ya Elimu wa Shirika la UNESCO, Bi. Jennifer Kotta pamoja na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Al Amin Yusuph.

Kuwapo kwa kijiji hicho ni matokeo ya mkataba uliotiwa saini kati ya UNESCO na kampuni ya elektroniki ya Samsung mwaka jana.

Katika makubaliano hayo yalitiwa saini na Mwakilishi mkazi Unesco nchini, Zulmira Rodrigues na Mkurugenzi wa Samsung Electronics nchini Tanzania, Mike Seo katika Kijiji hicho kitakuwa na shule yenye Tehama ikiwa na maunganisho ya intaneti, kiliniki ya kisasa ikiwa na kituo cha teknolojia ya mawasiliano yenye kuwezesha utabibu (Telemedicine) na jenereta linalotumia nguvu za jua kwa ajili ya kijiji hicho.

Mradi huo utawezesha UNESCO kuwapatia vijana wa Kimasai elimu kutokana na ukweli kuwa kwa utamaduni na kazi zao za ufugaji wamekuwa wakipata shida ya kupata elimu.
DSC_0096
Mkutano huo pia ulihudhuriwa na wataalam wa Elimu, Afya, Utamaduni na Kilimo kutoka Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro jijini Arusha. Kushoto pichani ni Mganga Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Dkt. Peter Kitenyi.

Kupitia kijiji hicho vijana wataendelea na masomo hata kama wanachunga mifugo yao.
Wakati wa utiaji saini Mkurugenzi wa Samsung Electronics nchini Tanzania alitaja miongoni mwa manufaa makubwa yatakayopatikana katika mradi huo wa kijiji cha digitali huko Loliondo ambayo ni pamoja na kuweza kupata nishati rahisi na iliyo rafiki kwa mazingira.

Alisema kwamba Afrika imekuwa mstari wa mbele katika uanzishaji wa vijiji vya digitali. Aidha kwa kitendo hicho Afrika inaonesha dunia ni kwa namna teknolojia inaweza kutumika kuleta mabadikliko chanya yanayotakiwa kwa ajili ya maendeleo ya wananchi waliopo vijijini.

Kijiji hicho cha Loliondo kitakuwa cha nne katika vijiji vya kidigitali barani Afrika.Inatarajiwa kwamba kijiji kingine kitajengwa mjini Zanzibar kwa ushirikiano wa UNESCO na Samsung Electronics mwaka huu.
DSC_0080
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akifafanua jambo kwa Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali wakati wa mazungumzo na mkuu wa wilaya hiyo kabla ya kuelekea kijiji cha Ololosokwani kwa ajili ya mkutano na wanakijiji wa kijiji hicho kabla ya kuwasili kwa mradi wa kijiji cha kidigitali mapema mwezi februari.
DSC_0092
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akielezea changamoto za miundo mbinu ya barabara kwa kutumia picha alizopiga akiwa njiani kuelekea kijiji cha Ololosokwan kupitia barabara ya Lake Natron kwa Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali.
DSC_0105
Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali akielezea jitihada zitakazofanywa na wilaya yake katika kuhakikisha miundo mbinu ya barabara inarekebishwa kuondoa usumbufu kwa magari mazito yenye vifaa vya kijiji cha digitali cha Ololosokwan yanapita bila kikwazo mapema mwezi februari.
DSC_0136
Wataalamu kutoka halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro, Unesco pamoja na Wizara ya afya wakitazama picha hizo kwenye kompyuta mpakato ya Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues ofisini kwa Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro.
DSC_0136

No comments: