Na:
Mwandishi Wetu
Fainali ya Mashindano ya mpira wa
miguu kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) inayojulikana kama
Airtel UNI255 iliyoshirikisha wanafunzi wote wa schools na Colleges zilizopo
chuo kikuu itarudiwa siku ya jumamosi ya tarehe 10/1/2015 kwenye viwanja
vya chuo kikuu cha Dar es salaam(UDSM) baada ya Fainali hiyo kushindwa
kumalizika na kukosa mshindi kutokana na Kiza kilichoingia na
kuleta mkanganyiko wa nani anastahili kuwa Bingwa katika mchezo uliofanyika
mwishoni mwa mwaka jana.
Fainali hiyo ambayo ilivikutanisha
vyuo vya Sayansi ya Jamii (College of Social Science) na Chuo cha Uhandisi na
Teknolojia (College of Engineering and Technology) hadi dakika tisini(90) za
mchezo zinamalizika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) timu
hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1.
Akizungumzia marudio ya fainali
hiyo, waziri wa michezo wa Serikali ya wanafunzi katika Chuo kikuu cha
Dar es Salaam, STANLRY JULIUS alisema kuwa michezo hiyo ilileta changamaoto kubwa sana
katika chuo hicho na kitendo cha kutopata mshindi kilitokana na kuchelewa
kuanza kwa fainali hiyo ambayo hata hivyo baada ya Uongozi wa chuo kukaa na
kutathmini waliamua mechi hiyo irudiwe ili kupata mshindi wa kwanza na wa pili
kwa kuwa timu hizo zitatakiwa kuungana na timu zingine za jiji la Dar es salaam
katika ligi ya kutafuta chuo bora katika mchezo wa mpira wa miguu.
“kikubwa tu ni kwamba tunaishukuru
kampuni ya simu za mkononi AIRTEL kupitia mpamgo wake wa UNI255 kwa kusapoti
michezo hii ya vyuo, bila shaka Tanzania kupitia shirikisho la mpira wa Miguu
Tanzania(TFF) linaweza pia kunufaika na michezo hii ya vyuo kwa kupata wacheza
watakaoisaidia Nchi kwenye timu ya Taifa”alisema STANLRY JULIUS
Kwa mujibu wa Waziri huyo wa serikali ya wanafunzi,
Mchezo huo wa fainali utafanyika kwenye viwanja vya chuo kikuu cha Dar es
salaam mapema kuanzia saa tatu kamili asubuhi na unatazamiwa kumalizika saa
tano na baada ya kumalizika kwa mchezo huo hafla ya kukabidhi zawadi itafanyika
kwenye tawi la chuo hicho Mabibo Cumpas na amesisitiza kwamba suala la usafiri
kwa wanafunzi ni bure na usafiri utakuwa mwingi wakati wote kwenda Mabibo na
kurudi chuo Kikuu kuanzia asubuhi hadi jioni.
Naye Meneja Uhusiano wa Airtel
Jackson Mmbando alisema kuwa kutokana na kukosa mshindi kwenye mchezo wa
fainali wao wakiwa ndo wadhamini wakuu walilitazama kwa namna ya pekee hivyo
wameamua kuongeza bajeti ingine ili kuhakikisha kwamba fainali hiyo inapata
mshindi wa kwanza na mshindi wa pili.
Michezo inaleta afya na ndiyo maana
tumeamua kutumia gharama nyingine tena ili kuunga mkonpo jitiada za chuo kikuu
cha UDSM kufanikisha michezo hii ya Vyuo,”alisema Jackson Mbando
Aidha katika kilele cha marudio ya
fainali hiyo Airtel imeandaa burudani mbali mbali ikiwemo mbio za Piki piki,
Mashindano ya Vipaji vya kuimba, kucheza, pamoja na wasanii akiwemo Roma
Mkatoliki, Shilole anaetamba na wimbo wake mpya wa Malele, ney wa mitego ambapo
hawa wataongozwa na DJ maarufu jijini Dj Zero
No comments:
Post a Comment