Tangazo

January 28, 2015

TBL YATOA MSAADA WA SH. MIL 45 ZA UCHIMBAJI KISIMA CHA MAJI ZAHANATI YA MJI MWEMA


 Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bi. Dorice Malulu (kulia), akikabidhi mfano wa Hundi ya Sh. Milioni 45, kwa Mganga Mkuu wa Zahanati ya Mji Mwema, Kigamboni, Bw. Richard Mwita, zilizotolewa na TBL kwa ajili ya ujenzi wa kisima cha maji. Wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Bodi, Bw. Omari Kombe (kushoto), Bi. Upendo Mwabulambo (wa pili kushoto) na Mwakilishi wa Mganga wa Manispaa ya Temeke, Bw. Shaidi Simba (wa pili kulia). (Na Mpigapicha Wetu)

Mwakilishi Mkuu wa Mganga wa Manispaa ya Temeke, Bw. Shaidi Simba (kulia), akimkabidhi Mhandisi Amiri Msangi mfano wa hundi ya milioni 45 zilizotolewa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa ajili ya kuchimba kisima cha maji kwenye Zahanati ya Mji Mwema. Katikati ni Mganga Mkuu wa Zahanati hiyo, Dkt. Richard Mwita, Mwenyekiti wa Bodi, Bw. Omari Kombe (kushoto) na Muuguzi, Bi. Upendo Mwabulambo. (Na Mpigapicha Wetu)

No comments: