Tangazo

February 3, 2015

DKT. NCHIMBI ASEMA CCM HAINA TATIZO LA KIMUUNDO WALA MFUMO

nchimbi 3
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe za Maadhimisho ya miaka 38 ya CCM, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songea, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza katika maadhimisho ya miaka 38 ya CCM, yaliyofanyika kitaifa juzi kwenye Uwanja wa Maji Maji mjini Songea, Mkoani Ruvuma.Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.

Na Mwandishi Wetu

Mwenyekiti wa maandalizi ya sherehe za maika 38 ya Chama Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni mbunge wa Songea mjini Dkt Emmanuel Nchimbi amesema kuwa chama chake kina kila sababu ya kushinda kwa kishindo kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu kwa kuwa kina mfumo na muundo imara.

Akizungumza muda mfupi baada ya maadhimisho hayo mjini Songea, Dkt Nchimbi ambaye pia ni mjumbe wa halmashauri kuu ya chama hicho alisema kuwa chama chake hakina tatizo la kimfumo wa muundo na kuongeza kuwa ushindi ni lazima.

“Chama hakina tatizo la muundo wala mfumo na tutakachofanya ni kubadilisha mikakati tu ili kujihakikishia ushindi katika uchaguzi ujao,” alisema
nchimbi 4
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe za Maadhimisho ya miaka 38 ya CCM, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songea, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe katika maadhimisho ya miaka 38 ya CCM, yaliyofanyika kitaifa juzi kwenye Uwanja wa Maji Maji mjini Songea, Mkoani Ruvuma katikati ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho.

Aliongeza, “Kwa kwa kaida hakuna mkakati unadumu. Mar a zote mikakati hubadilika kulingana na mazingira na hiki ndicho tutakachokifanya,”

Akizungumzia kuhusu kauli ya mwenyekiti wa chama hicho Rais Jakaya Kikwete kuwataka viongozi wa chama kuwatembelea wanachama na kushawishi wanachama wapya, alisema CCM ni chama kikubwa na ndani yake wapo viongozi waliolala ambao mwenyekiti wa taifa aliwakumbusha kuamka na kufanya kazi.

“Chama hakiwezi kuwa na maisha marefu kama viongozi katika ngazi zote ha hawajitumi. Katika jeshi kubwa kama hili la CCM wapo watu ambao lazima wasukumwe na ndiyo ahwa mwenyekiti wetu wataifa aliwasukuma kupitia hotuba yake.

Hawa wanatakiwa kuamka na kuanza kufanya kazi kwa bidii ili kukiwezesha chama kushinda kwa kishindo kama ambavyo kimekuwa kikishinda tangu kuanza kwa siasa za vyama vingi,” alieleza
nchimbi 2
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe za Maadhimisho ya miaka 38 ya CCM, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songea, Dk. Emmanuel Nchimbi (kulia) akiteta jambo na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.

Dkt Nchimbi aliishukuru halmashauri kuu ya chama kwa kuweza kuuchagua mkoa wa Ruvuma kwa ajili ya maazimisho ya miaka 38 ya chama hicho na kueleza kuwa kwa miaka mingi Ruvuma imekuwa ngome imara ya CCM.

Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho alisema kuwa alisema kuwa chama chake kimeshaanza kujipanga kwa ajili ya uchaguzi mkuu .

“Nimeshawaagiza viongozi wa chama katika ngazi ya mkoa na wilaya kuanza vikao kwa ajili ya na kuweka mikakati thabiti ya ushindi katika uchaguzi mkuu ujao,”

Alieeleza kuwa, chama katika mkoa wake tayari kilishaanza mikakati ya kujitegemeza ikiwa ni kufuata agizo la mwenyekiti wa taifa ambapo tayari kimejipanga vyema kuendeleza vyanzo vyake vya mapato pamoja na kuanzisha vyanzo vipya kwa ajili ya kukifanya kujitegemea.
nchimbi 1
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe za Maadhimisho ya miaka 38 ya CCM, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songea, Dk. Emmanuel Nchimbi (kulia) akijadiliana jambo na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula (katikati) pamoja na Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana.

No comments: