Tangazo

March 31, 2015

NACTE INTER COLLEGE CHAMPIONSHIP TANZANIA 2015



Katibu Mkuu wa Mashindano ya Vyuo vilivyosajiliwa na NACTE TANZANIA,  Waziri wa Michezo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM), Ladslaus Tumbu (kulia) na Katibu Msaidizi wa Michuano hiyo, Waziri wa Michezo kwenye Chuo cha Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Samweli Samweli (wa pili kulia), wakikabidhi Kombe linaloshindaniwa na Vyuo mbali mbali Kanda ya Dar es Salaam(Mashariki) kwa Viongozi wa NACTE, Msaidizi wa Mkurugezi, Alex Mkondola (wa kwanza kushoto) na Mwanasheria Mkuu NACTE Cexemary Mize (wa Pili kushoto), wakati wa hafla ya kukabidhi Kombe hilo la Michuano ya NACTE TANZANIA, lililotolewa na Kampuni ya Simu za Mkononi VODACOM Tanzania, Michuano hiyo inafunguliwa April 18 kwenye Viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM).
XXXXXXXXXX

Kamati ya Mashindano ya Michezo ya Vyuo Tanzania( NACTE INTER COLLEGE CHAMPIONSHIP TANZANIA 2015), imekabidhi kombe la Michezo hiyo kwa Taasisi ya Elimu ya Vyuo nchini Tanzania, NACTE baada ya kamati hiyo kupokea kombe hilo kutoka kampu ni ya Simu ya VODACOM TANZANIA, lililotplewa kwa ajili ya michuano hiyo ya vyuo vya Tanzania iliyoanza November Mwaka jana jijini Dar es Salaam.

Akizungumza makao makuu ya Wizara(NACTE)  Msaidizi wa Mkurugezi, Alex Mkondola alisema kuwa ni heshima ya pekee kwa NACTE kutokana na Uwepo wa michezo hiyo inayoshirikisha vyuo mbali mbali vilivyosajiliwa na NACTE nchini Tanzania.

"Wanafunzi wengi vyuoni wamekuwa wakizungumzia hitaji lao la kutaka michezo ya pamoja kwa vyuo vya elimu ya kati na vyuo vya elimu ya juu kushindana katika kutafuta bingwa wa kila mchezo, hivyo fulsa hii ni yao na sisi jukumu letu ni kuhakikisha kwamba michezo hii inafanyika kupitia wasimamizi mwakuu tuliowapa ridhaa ya kuwa waandaaji kampuni ya Miss Demokrasia Tanzania.

Ni matumaini yetu kwamba sasa vijana mbali mbali watashiriki kujiandikisha kwa ajili ya kuonyesha Vioaji vyao bila kubagua aina ya mchezo, tunashukuru wenzetu wa VODACOM wao kuwezesha Kombe hili kubwa kwa ajili ya mchezo wa mpira wa Miguu, lakini hata hivyo michezo yote itashiriki isipokuwa tunapenda kuwasisitiza wakuu wa vyuo kuwapa mwanya huo vijana wao waweze kuwakilisha taasisi zao katika kuwania tuzo hizi ambazo zinatofautiana kutokana na ubora wake, sisi kama NACTE tumeona ni jambo la kupendeza kuwapo kwa michezo hii kwenye vyuo vya elimu ya kati na hata elimu ya juu ili mradi wawe wanachama wetu, tunapenda tu kutoa angalizi kwa wakuu wa vyuo, kwamba tusingependa wanamichezo wao kuonyesha nidhamu mbaya michezoni, maana lengo kubwa la michezo hii ni kujenga mahusiano mema na siyo kuleta mgongano, na pia ni kwa ajili ya kujenga afya zao wenyewe maana michezo inawajenga katika mambo mengi hivyo waitumie fulsa hii kujenga mahusiano mazuri miongoni mwao, tuwashukuru wadhamini wote.

Waliojitokeza kusaidia baadhi ya mahitaji kwa ajili ha kufanikisha michezo hii ya vijana wetu, na pia tuwatake wawezeshaji wengine kujitokeza katika kusaidia wakati wote wa mashindano, kwa sasa NACTE imepanua wigo maana tunayo matawi 6, Kanda ya Mwanza, Arusha, Mbeya, Dodoma, Zanzibar na Dar es Salaam, tunahitaji kupata bingwa wa Tanzania kwa College zilizo mwanachama wetu, Siku ya ufunguzi tunaomba wakuu wa vyuo vyote vya Dar es Salaam na maeneo ya jirani, kuruhusu wanafunzi kuhudhulia kwenye Kongamano kubwa la Ufunguzi ambapo wanafunzi wote watapata fulsa ya kujiandikisha kwa ajili ya kushiriki kwenye fani mbali mbali za vipaji vyao ikiwa ni pamoja na Dibate" alisema Alex Mkondola

Michezo hiyo inazinduliwa April 18 kwenye viwanja vya Chuo kikuu cha Dar es Salaam, ambapo jumla ya timu 18 zitashiriki kwenye ligi hiyo ambayo imeingia hatua ya pili baada ya hatua ya kwanza ya makundi ya mtoano kumalizika ambapo jumla ya vyuo 115 vilishiriki kabla ya hatua hii ya 18 bora.

Wadhamini waliokotpokeza mpaka sasa ni Vodacom Tanzania, Coca Cola,  EQUITY Bank, P.S.I, TBL, TTB, White Dent, Fastjet, , MSD, N.H.I.F, CLOUDS MEDIA GROUP, FREE MEDIA, Tanzania Daima, MLIMAN TV & Radio, Viasat 1 Tanzania( TV-1), Global Publishers, Michuzi Media Group, MpaluleBlog, Event World, DACICO, Mliman Professional, Njuweni Institute of Hotel, Catering & Tourism Management, Zinduka Development Initiatives Forum,Dkt Mwaka, BIG BON, No-saspect Berbershop,CXC Tours, Omari Mawamba na Mlonge By Makai. 

No comments: