Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Sekretarieti leo kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi mjini Dodoma, tarehe 23 Mei 2015.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kamati Kuu katika kikao
chake cha tarehe 22/05/2015 mjini Dodoma pamoja na mambo mengine
imepokea na kutafakari kwa kina taarifa ya maandalizi ya mchakato wa
kupiga kura ya maoni kwa Katiba inayopendekezwa.
Baada
ya kutafakari na kwa kuzingatia changamoto mbalimbali zilizojitokeza
katika maandalizi hayo, Kamati Kuu ya CCM inaishauri serikali kwa
kushauriana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, wakizingatia changamoto
zilizopo na hali halisi ya mchakato huu, kutafuta njia muafaka ya
kulishughulikia na kulihitimisha jambo hili kwa maslahi mapana ya Taifa
letu.
Imetolewa na:-
Nape Moses Nnauye
Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM (T).
23/05/2015
No comments:
Post a Comment